Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:24

Biden na Harris kuanza kampeni Jumatano Delaware


Makamu wa Rais wa zamani Jeo Biden na mgombea mwenza Kamala Harris.
Makamu wa Rais wa zamani Jeo Biden na mgombea mwenza Kamala Harris.

Mgombea urais wa Marekani wa chama cha Demokrat Joe Biden, na mgombea mwenza Kamala Harris aliyetangazwa hapo Jumanne wanatarajia kufanya kampeni ya pamoja kwa mara ya kwanza Jumatano.

Tayari wameshaunda timu ya kuelekea kuleta upinzani kwa rais Donald Trump na makamu wake Mike Pence katika uchaguzi wa Novemba, 2020.

Time ya Kampeni ya Biden na Harris imeeleza wagombea hao wataongea katika mji wa Wilmington, katika jimbo la Delaware, kuhusu kufanyakazi kwa pamoja kurejesha imani ya taifa lao.

Wagombea hao wanaazma kuzipigania familia za wafanyakazi ili kulipeleka taifa mbele.

Biden alimtangaza Harris Jumanne, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi na Mmarekani mwenye asili Asia Kusini kuchaguliwa kuwa katika tiketi muhimu ya chama cha Demokratik kugombania nafasi ya umakamu wa rais.

XS
SM
MD
LG