Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:25

Tanzania yapiga marufuku kurusha matangazo ya kimataifa bila ya kibali


TCRA
TCRA

Vyombo vya habari nchini Tanzania Radio na Televisheni vimepigwa marufuku kuanzia sasa kurusha matangazo ya vyombo vya kimataifa hadi pale vitakapo pata kibali maalumu kutoka serikalini.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni mpya zilizopitishwa na Mamlaka ya mawasiliano nchini humo, TCRA hivi karibuni.

Tangazo lililotolewa na mamlaka hiyo linasema kwamba kanuni hizo mpya zimeanza kutumika tangu Julai mosi mwaka 2020, na kwamba radio na televisheni nchini zinazoendelea kurusha matangazo ya kimataifa vitakuwa vinaeendelea kutenda makosa kurusha matangazo hayo bila Kigali.

Kanuni hizo zinasema radio na televisheni vinavyotaka kuanzisha ushirikiano na vyombo vya nje kwa kupeperusha matangazo yake kabla ya kuendelea na mpango huo vinapaswa kwanza kuomba kibali kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa kuandika barua kwa mkurugenzi wake mkuu vikielezea sababu ya kutaka kuwa na ushirikiano huo na jinsi utakavyo endeshwa.

Kanuni hizo hazijasema lolote kama maombi hayo yatachukuwa muda gani kujibiwa mbali ya kusisitiza kwamba mkurugenzi mkuu wa tcra ana mamlaka ya mwisho kuhusu kuwepo kwa mashikiano hayo.

Kwa miaka mingi sasa mashirika ya kimataifa kama vile VOA, DW na BBC yamekuwa tegemeo la wasikilizaji wengi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Kwa miaka mingi sasa mashirika ya kimataifa kama vile VOA, DW na BBC yamekuwa tegemeo la wasikilizaji wengi katika ukandahuu wa Afrika Mashariki.

Vyombo hivi vimekuwa vikifanya upashaji habari usioengemea upande wowote na vimekuwa vikitoa taarifa zinazo kosoa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu na kutofuata misingi ya utawala bora.

Ujio wa kanuni hizo huenda ukaweka kizingiti kingine kwa mashirika ya kimataifa kupenyeza taarifa zake kwa wasikilizaji wake katika eneo hili na tayari kanuni hizo zimeanza kupigiwa kelele na wafutiliaji wengi wa mambo, vyama vinavyo husika na masuala ya habari, wanaharakati pamoja na wachambuzi wa mambo wanasema kwamba kanuni hizo zinazidi kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

Pascal Mayala mwandishi na mtangazaji wa siku nyingi ambaye pia ni mwanasheria anasema njia pekee ya kujinasua na kanuni hizo mpya ni kuanzisha majadiliano na serikali yenyewe.

“Baadhi ya radio maudhui yake siyo mazuri. Lakini zile Public Broadcasting stations kama BBC, DW halafu kuja kuwaambia wametangaza kitu na unataka kumshtaki, kitu kimetangazwa na DW ama voice of america ama BBC, kuja kumshtaki mtu wa Radio Free Afrika, huu ni uonevu kupita maelezo," amesema.

"Waandishi tukiendelea kunyamaza haitatusaidia. Iliobakia ni waandishi tusimame kwa pamoja siyo kupinga serikali Tujenge hoja za msingi zinazokubalika halafu tuziwasilishe serikalini, naamini serikali yetu ni sikivu na itatusikiliza," ameeleza. Mayala.

TCRA inasema kwamba kanuni hizo mpya zimeletwa ili kujazilizia mapungufu yaliyokuwepo katika sheria ya awali ya maudhui ya vyombo vya habari vya redio na televisheni ya mwaka 2018 ambayo haikujumuisha kipengele hicho.

Duru za habari zinasema kwamba baadhi ya vyombo hivyo vya habari tayari vimeanza kutekeleza kanuni hiyo kuanzia leo.

Vyombo hivyo ambavyo vimekuwa vikipeperusha matangazo hayo leo viliendelea na vipindi vyake vingine vikitoa burudani ya muziki bila kujiunga na mashirika hayo ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG