Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:45

Mgogoro kuhusu safari za Tanzania bado kutatuliwa, yasema Kenya Airways


Ndege ya shirika la Kenya Airways.
Ndege ya shirika la Kenya Airways.

Shirika la ndege la Kenya Airways linasema kuwa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania haijabatilisha uamuzi wa kufuta kibali cha kuziruhusu ndege zake kusafiri nchini humo takriban wiki moja baada ya Waziri wa Uchukuzi wa Kenya James Macharia kueleza kuwa nchi hizo mbili zimefikia makubaliano.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirika hilo la Kenya, Allan Kilavuka, ameeleza kuwa usimamizi wa KQ unasubiri jibu kutoka kwa serikali ya Kenya kwa sababu bado hawajapata idhini ya kusafiri Tanzania.

Takriban wiki moja baada ya serikali ya Kenya kutangaza kuwa imefanya mazungumzo na Tanzania kusuluhisha mgogoro ulioibuka Ijumaa wiki iliyopita baada ya Tanzania kutangaza kufuta ndege za shirika la ndege la Kenya Airways(KQ) kufanya safari zake humo katika viwanja vyake vya ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar, Kenya Airways inasema bado hamna jibu ya kufanya safari nchini humo.

Afisa Mkuu mtendaji wa shirika hilo Allan Kilavuka ameeleza VOA kuwa shirika hilo linasubiri maelekezo kutoka kwa serikali ya Kenya kujua utaratibu uliopo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:22 0:00

Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya James Macharia wakati akizindua safari za ndege za Kenya Airways to nchi 30 wiki iliyopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) alieleza kuwa amefanya mazungumzo na Waziri wa Kazi, uchukuzi na mawasiliano nchini Tanzania Isack Aloyce Kamwelwe na kukubaliana mgogoro huo.

Hata hivyo, Bw Kilavuka anakariri kuwa Kenya Airways haiwezi kufanya chochote ila kusubiri jinsi mgogoro huo unavyosuluhishwa na mamlaka husika za serikali hizi mbili.Lakini anaeleza kuwa kusitishwa huko kuna athari kubwa kwa Kenya Airways.

Hatua hiyo ya Tanzania ilifuatia tangazo la serikali ya Kenya kutoiorodhesha nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi 11 ambazo wasafiri wake wanaruhusiwa kuwasili Kenya wakati usafiri wa kimataifa unaporejea.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari Ijumaa wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania (TCAA), Hamza Johari alisema serikali ya Tanzania imesimamisha mara moja safari za ndege za shirika la Kenya Airways kutoka Nairobi kutua viwanja vyake kufuatia tangazo la Kenya kuiacha nje ya nchi zinazoruhusiwa kufanya safari humo.

Hata hivyo siku moja baadaye, Kenya ilitoa ufafanuzi kuwa haijapiga marufuku ndege za Tanzania kuingia nchini mwake hata kama si miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa ndege zake kuingia anga ya Kenya.

Kenya Airways ilirejelea safari za ndege za kimataifa Agosti mosi mara ya kwanza baada ya kusitisha safari hizo Machi mwaka huu kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

-Imetayarishwa na Kennedy Wandera, VOA, Nairobi

XS
SM
MD
LG