Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:13

Mawaziri watatu wajiuzulu Lebanon


Waandamanaji wakiwatupia polisi mawe Agosti 9, 2020, kufuatia mlipuko wa Jumanne Agosti 4 ulioharibu eneo la Beirut, Lebanon.
Waandamanaji wakiwatupia polisi mawe Agosti 9, 2020, kufuatia mlipuko wa Jumanne Agosti 4 ulioharibu eneo la Beirut, Lebanon.

Waziri wa Sheria wa Lebanon, Marie-Claude Najm, amejiuzulu, ni waziri wa tatu kuachia madaraka baada ya mlipuko mkubwa wa wiki iliyopita mjini Beirut.

Waziri wa Mazingira, Demanios Kattar alijiuzulu Jumapili jioni, akisema serikali “imeelemewa.” Waziri wa Habari, Manal Abdel-Samad amejiuzulu mapema Jumapili.

Mawaziri kadhaa wanaripotiwa kuwa wanafikiria kujiuzulu. Baraza la Mawaziri litakutana siku ya Jumatatu.

Wakati huohuo, wabunge wasiopungua nane wametangaza wanajiuzulu wakati bunge litakutana baadae wiki hii.

Viongozi wa dunia wameahidi Jumapili kuchangia takriban dola milioni 300 kwa ajili ya Lebanon ili kuisaida kujikwamua kutokana na athari za mlipuko wa Beirut.

Zaidi ya viongozi 30, wakiongea katika mkutano uliofanyika kwa njia ya simu chini ya uwenyekiti wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, wamesema “msaada huo uwafikie mara moja, uwe wa kutosha na unalingana na mahitaji ya watu wa Lebanon… na ufikishwe moja kwa moja kwa wananchi wa Lebanon kwa ufanisi na uwazi.”

Fedha hizo hazitawekewa masharti ya kisiasa au mageuzi ya kitaasisi, ofisi ya Macron imesema.

Lakini ahadi hizo za michango zimetolewa kwa ajili ya msaada wa muda mrefu ambao utategemea na mabadiliko yatakayo fanywa na mamlaka husika, kasri ya Elysee imeeleza.

Mataifa yenye nguvu dunaini yamesisitiza kuwepo uwazi katika matumizi ya msaada huo, wakichelea kupeleka msaada kwa serikali ambayo wananchi wengi wa Lebanon wanaona kama ni yenye ufisadi na wakieleza wasiwasi wao juu ya ushawishi wa Iran katika serikali hiyo kupitia kikundi cha Mashia cha wapiganaji wa Hezbollah.

XS
SM
MD
LG