Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:11

Radio Guinea-Bissau zasitisha matangazo kulaani shambulizi


Wanachama wa Jumuiya ya Waandishi na Mafundi mitambo nchini Guinea-Bissau, wakionyesha sikitiko la shambulizi dhidi ya Radio Capital FM hook Bissau, Guinea-Bissau, Agosti 6, 2020.
Wanachama wa Jumuiya ya Waandishi na Mafundi mitambo nchini Guinea-Bissau, wakionyesha sikitiko la shambulizi dhidi ya Radio Capital FM hook Bissau, Guinea-Bissau, Agosti 6, 2020.

Vituo vingi vya radio nchini Guinea-Bissau vilisitisha matangazo kwa masaa 24 Alhamisi kuonyesha mshikamano baada ya kituo kimoja cha Radio Capital FM kushambuliwa.

Alfajiri Julai 26, kikundi cha wanaume waliokuwa wamevaa nguo za polisi na wakiwa wana silaha za kivita waliingia katika ofisi za Capital FM katika mji mkuu, Bissau, naibu mkurugenzi Sabino Santos aliiambia Sauti ya Amerika VOA.

Alisema vifaa vya kituo hicho – ikiwemo kifaa cha kurushia matangazo, kuchanganya sauti na kompyuta – viliharibiwa.

Tangu wakati huo kituo hicho kimekuwa kikitangaza habari na maudhui nyingine kupitia mtandao wa Facebook.

Vituo kadhaa binafsi vya radio katika mji huo mkuu na vituo 23 vya radio za kijamii kote katika nchi hiyo iliyoko Afrika Magharibi vilisitisha matangazo ya habari na programu nyingine.

“Tunataka tuonyeshe kwamba sekta ya habari ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,” amesema Diamantino Domingos Lopes, katibu mkuu wa jumuiya ya wafanyakazi.

“Tumetaka tusitangaze siku moja kuonyesha kukerwa kwetu na kile kinachoendelea katika sekta hii.”

Lopes ameelezea shambulizi hilo dhidi ya Capital FM kuwa “ni ukiukaji uliopindukia wa uhuru wa kujielezea.”

Jumuiya hiyo ilikuwa imetaka mamlaka husika nchini Guinea-Bissau ifikapo Jumatano wawe wamejibu madai yao kwa wahusika kuwajibishwa na kufikishwa mahakamani.

Polisi wamewaambia waandishi kuwa wanaendelea na uchunguzi, ingawaje hakuna tamko rasmi lililotolewa hadi sasa na walioshambulia kituo hicho hawajaweza kutambuliwa.

Shambulizi katika kituo cha Capital FM lililaaniwa na maafisa wa serikali ya Guinea-Bissau ikiwemo kauli ya waziri katika ofisi ya rais, Mamadu Serifo Djaquite.

Pia washirika watano wa kimataifa wa nchi hiyo wamelaani shambulizi hilo ikiwemo: Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya nchi zinazoonegea Kireno, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

VOA au maudhui yake haionekani kuwa ni sababu ya shambulizi hilo, kwa mujibu wa tamko la mkurugenzi wa mahusiano ya umma VOA.

Kituo hicho kilikuwa kinapokea vitisho kila mara kwa miezi kadhaa kwa sababu ya progamu zake, mmiliki wa kituo na mkurugenzi Lassana Cassama ameiambia kamati ya kuwalinda waandishi (CPJ) yenye makao yake makuu New York mapema wiki hii.

Cassama, ambaye pia anaripoti katika idhaa ya Kireno ya VOA, amesema vitisho hivyo vilivyokuwa vikitolewa walifahamishwa polisi.

Mwezi June, Serifo Camara, mhariri wa Capitol FM, alishambuliwa na watu wenye silaha nje ya kituo cha radio hiyo akitoka kutangaza habari za usiku kituoni.

Cassama ameiambia CPJ kuwa itagharimu takriban euro 38,000 au ($44,663) kutengeneza vifaa vilivyo haribiwa.

XS
SM
MD
LG