Baada ya wiki kadhaa za mashauriano ya faragha, ambayo yaliongezeka kasi Jumatano kwa ziara ya siri ya ujumbe wa Israeli mjini Khartoum, Rais Donald Trump alitangaza makubaliano ya kurejea mahusiano hayo Ijumaa huko White House.
“Mabadiliko ya kustaajabisha!” Netanyahu alisema katika tamko lake lililokuwa katika lugha ya Kihibrania.”
“Leo Khartoum inasema inakubali amani na Israeli, ndiyo inatambua uwepo wa Israeli na kurejesha mahusiano ya kawaida na Israeli.”
“Wajumbe kutoka Sudan na Israel watakutana hivi punde kujadili ushirikiano katika nyanja nyingi, miongoni mwao kilimo, biashara na maeneo mengine muhimu,” ameongezea.
Hamas, hata hivyo, imekosoa makubaliano hayo na kuyaita “dhambi ya kisiasa.”
Mkataba huo, “unamadhara kwa watu wetu wa Palestina na juhudi zao za kutafuta haki, na pia unamadhara kwa maslahi ya kitaifa ya Sudan,” msemaji wa Hamas Hazem Qassem alisema.
“Unamnufaisha Netanyahu tu,” aliongeza.
Tamko rasmi la Hamas limewataka wananchi wa Sudan kukataa kile walichosema ni “makubaliano ya fedheha”.
The presidency of Palestinian leader Mahmud Abbas, based in the Israeli-occupied West Bank, joined the condemnation.
Ofisi ya kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas, iliyoko katika eneo linalokaliwa kimabavu la Ukanda wa Magharibi imeungana na wengine kulaani mkataba huo, tamko hilo limeeleza.
Imeongeza kuwa “hakuna mtu aliye na haki ya kuwazungumzia watu wa Palestina na harakati za Palestina”.
Sudan ni nchi ya tatu ya Kiarabu tangu Agosti kutangaza kurejesha mahusiano yao na Israel, baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain kufanya hivyo.