Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Israeli: Hamas na Fatah waungana kupinga ujenzi kwenye ukingo wa Magharibi


Viongozi wa Hamas, akiwemo Saleh al Arouri, katika moja ya mikutano.
Viongozi wa Hamas, akiwemo Saleh al Arouri, katika moja ya mikutano.

Makundi hasimu ya Wapalestina ya Fatah na  Hamas Alhamisi yaliahidi kuungana pamoja dhidi ya mipango ya Israel ya ujenzi huko Ukingo wa Magharibi katika mkutano wa nadra wa pamoja, ikiwa ni dalili ya kuibuka kwa mvutano kati ya Israel na Washington juu ya mradi huo.

Uhusiano kati ya kundi la Fatah linalodhibiti eneo la Ramallah ambalo ni makao ya mamlaka ya Wapalestina, na kundi la kiislamu la Hamas ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza umegubikwa na migawanyiko kwa zaidi ya muongo mzima.

Mkutano wa pamoja na waandishi wa habari uliubeza mpango wa amani weye utatanishi wa Rais Donald Trump wa Marekani, ambao unafungua njia kwa Israeli kuvamia eneo inalolikalia kimabavu huko Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na makazi ya walowezi wa kiyahudi ambayo yanaonekana kuwa si halali kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

"tutaweka hatua zote muhimu kuhakikisha umoja wa kitaifa, katika juhudi dhidi ya uvamizi, afisa mwandamizi wa Fatah, Jibril rajub alisema mjini Ramallah katika mkutano na wanahabari, ambapo pia afisa wa Hamas, Saleh alArouri alizungumza kwa njia ya video kutoka Beirut.

“Tangazo la kuvamia lina maana kuwa risasi imepigwa juu ya kuundwa kwa taifa la wapalestina, na hii ina maana ni tangazo la vita kwetu sisi, na leo sote tumekutana pamoja kama Fatah, Hamas na kila mtu mwingine, kujadili na kuchukua uamuzi ambao utakuwa ni muafaka kwa tabia hii ya ukaliaji wa kimabavu, ambao ni adui yetu. Leo tunataka kuzungumza kwa sauti moja,” alisema Rajub.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa serikali ya ushirika wa mrengo wa kati alipanga Alhamisi kuwa ni siku ya kuanza utekelezaji wa mapendekezo ya Trump.

Lakini mpango wa Marekani, uliozinduliwa mwezi Januari, pia unataka uingiaji wowote uwe sehemu ya mpango mkubwa wa amani, ikiwemo mashauriano ya kuundwa kwa taifa la Palestina kwenye eneo la takriban asilimia 70 ya ukingo wa magharibi unaounganisha Gaza.

Mbali ya Marekani, jumuiya ya kimataifa imetoa sauti kwa kauli moja juu ya upinzani dhidi ya hatua ya upande mmoja ya Israel.

Netanyahu amesita kutoa tangazo ambalo linaweza kuleta malumbano siku ya Jumatano.

Watalaamu wanasema kuna ushahidi uliojitokeza kwamba mpango wa Netanyahu wa kusonga mbele hauenda ni sawa na ule wa Washington.

Saleh al Arouri afisa wa Hamas anasema kwamba ni wajibu wao kutoruhusu mpango huo kutekelezwa.

“Tunasonga mbele katika kufanikisha mradi wetu wa kitaifa na siyo kuruhusu uvamizi kufanikisha kutokemezwa na kuendeleza mradi. Tusikae kimya, tusipitishe wala tusikubaliane na hili,” alisema Arouri.

Waziri wa ulinzi wa Israel na waziri mkuu mbadala Benny Gantz, ambaye anatarajiwa kuchukua uongozi kama waziri mkuu mwezi Novemba mwaka 2021, alielezea wasi wasi wake kuhusu kuchochea mivutano ya kieneo na kusema uingiaji katika eneo hilo ni vyema usubiri mpaka janga la virusi vya corona lidhibitiwe.

XS
SM
MD
LG