Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:09

Hisia tofauti juu ya pendekezo la amani la Rais Trump ulimwenguni


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akiwana Rais wa Marekani Donald REUTERS/Joshua Roberts
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akiwana Rais wa Marekani Donald REUTERS/Joshua Roberts

Akiwa na matumaini ya kuleta “chomozo jipya la amani Mashariki ya Kati,” Rais wa Marekani Donald Trump alizindua mpango wake wa amani kwa ajili ya eneo hilo Jumanne kwa kushirikiana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wakiwa bega kwa bega.

“Dira yangu inawasilisha fursa ya maslahi kwa pande zote mbili, suluhisho la uhakika la mataifa mawili ambalo linatatua hatari ya taifa la Palestina kwa upande wa usalama wa Israeli,” Trump amesema akiwa White House chumba cha East Room.

Mwakilishi wa Wapalestina

Kitu kilichokuwa wazi ni kutokuwepo kwa mwakilishi wa Wapalestina, ambao umekataa mpango huo wa amani hata kabla ya kupata fununu za pendekezo hilo la kurasa 80, na ambao walikuwa hawajahusishwa katika mazungumzo juu ya mpango huo.

“Jerusalem haiwezi kuuzwa. Haki zetu zote haziwezi kuuzwa na siyo za kujadiliwa. Na mpango wako, hujuma hiyo, haitapitishwa,” Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema katika maelezo yake yaliyorushwa na televisheni akiyaelekeza kwa Trump kutoka Ramallah Ukingo wa Magharibi

Kizingiti cha muda mfupi

Trump anaona hatua hii ya awali ya kukataliwa mpango huo kama ni kizingiti cha muda na kuwaambia wale waliokuwa katika East Room kuwa alituma barua kwa Abbas, akimwambia kama atachagua “njia ya amani, Marekani na nchi nyingine nyingi, watakuwa pamoja naye. Tutakuwa na nyinyi kuwasaidia kwa njia nyingi mbalimbali.”

Kukubali mpango huu kutapelekea uwekezaji wa kutoka nje ya Palestina wa dola za Marekani bilioni 50, kupatikana ajira milioni moja kwa Wapalestina kwa zaidi ya muongo mmoja na kuongezeka mara mbili au tatu ya pato la ndani la taifa la Palestina

Ulimwengu wa Kiislam

“Huu ni wakati muwafaka kwa ulimwengu wa Kiislam kurekebisha makosa yao waliofanya mwaka 1948 ilipokuwa imeamua kulishambulia taifa jipya la Israel badala ya kulitambua,” amesema Rais Trump.

Misri, nchi moja wapo iliyokuwa imetangaza vita dhidi ya Israeli wakati ule, haijakataa dira ya Trump.

Misri yaridhia mpango wa Trump

Misri imeeleza kuridhia juhudi zinazoendelea kufanywa na Marekani kufikia suluhisho la kina na la haki juu ya mgogoro wa Palestina, limeeleza shirika la habari la Mashariki ya Kati mjini Cairo.

“Jordan inawafiki kila juhudi ya kweli inayolenga kufikia suluhisho la kina na la haki ambalo wtu watalikubali,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi amesema katika tamko lake.

Mabalozi wa nchi za Kiarabu

Pia waliokuwepo katika chumba cha East Room wakati wa uzinduzi wa mpango wa Trump wa amani ni mabalozi wa Bahrain, Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu.

“Ni furaha ilioje kuwa na wewe hapa,” Netanyahu alisema. “Na ishara muhimu ya wakati huu.”

Tamko la Saudi Arabia

Wachambuzi walisema tamko la hadharani kutoka Riyadh, linalopeleka ujumbe wa kuunga mkono mpango wa Trump, utalipa jambo hilo uzito zaidi, kwa kuwa Ufalme wa Saudi Arabia ni ngome yenye nguvu ya waislamu wa dhehebu la Sunni.

Baadae siku ya Jumanne, Saudi Arabia ilitoa tamko, lililosema, “Kufuatia tangazo la (Marekani), serikali ya Saudia inasisitiza kuwa inaunga mkono juhudi zote zinazolenga kufikia suluhisho la kina na la haki kwa ajili ya harakati za Wapalestina.”

Saudi Arabia inaridhishwa na “juhudi za uongozi wa Rais Trump kuandaa mpango kabambe wa amani kati ya Wapalestina na Waisraeli,” tamko limesema.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu

Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit amesema Jumatano kuwa kwa kusoma mpango huo mara ya kwanza unaonyesha kutokuwepo kwa kiasi kikubwa haki ya kikweli ya Wapalestina, lakini jumuiya hiyo inatafakari vizuri suala hilo na inaunga mkono juhudi zozote za kufikia amani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema pia inaliangalia pendekezo hilo kwa karibu ikisisitiza umuhimu wa suluhisho la kuwepo mataifa mawili ya Israeli na Palestina.

Pendekezo la Trump

Trump anapendekeza kuwepo taifa la Palestina lakini lisilokuwa na utawala kamili – kuongezwa maradufu kwa ardhi wanayoishi Wapalestina – na Israeli kuendelea kushikilia theluthi ya Ukingo wa Magharibi uliokuwa na mgogoro.

Serikali ya Isreali hivi sasa inajitayarisha kupiga kura Jumapili kwa ajili ya kuendelea kulikalia bonde la kimkakati la Jordan na makazi yote ya Israeli katika Ukingo wa Magharibi.

XS
SM
MD
LG