Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:54

Omani yasema itafungua ubalozi ukanda wa Magharibi wa Palestina


Sultan Qaboos bin Said
Sultan Qaboos bin Said

Omani imesema Jumatano inapanga kufungua ubalozi mpya katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel Ukanda wa Magharibi na kwamba ujumbe wa wizara yake ya mambo ya nje utakwenda Ramallah kwa ajili ya ufunguzi huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters nchi hiyo ilitangaza uamuzi huo wakati Washington ikizindua mpango wa kiuchumi ambao inasema utakuwa ni msingi wa amani kwa Israeli na Palestina. Lakini Wapalestina na nchi nyingi za Kiarabu zimesema hatua hiyo haina faida bila ya kuwepo suluhisho la kisiasa.

“Kwa kuzingatia msaada wa Oman kwa ndugu zetu wa Palestina, imeamua kufungua ubalozi mpya kwa ajili ya Wapalestina katika kiwango cha ubalozi,” wazara ya mambo ya nje imeposti kwenye ujumbe wa twitter.

Ujumbe kutoka wizara ya mambo ya nje utaelekea Ramallah kuanza taratibu za kufungua ubalozi huo,” ujumbe wa tweet uliongeza.

Chanzo cha habari ambacho kinaelewa uamuzi huu kimesema kuwa Oman ilifunga ubalozi wake Gaza kufuatia shambulio la mabomu lililofanywa na Israel mwaka 2006 katika eneo la ardhi hiyo, lakini iliendeleza ushirikiano wa karibu na serikali ya Palestina.

Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha ukombozi cha Palestina, PLO, Hanan Ashrawi amepokea kwa furaha uamuzi huo na utambuzi wa namna yeyote ule wa taifa la Palestina.

“Ni matumaini yangu ubalozi utasaidia kuwaelimisha serikali ya Omani kuhusu uhalisia wa vitendo vya uvamizi vya Israeli,” Ashrawi ameongeza, akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari Jumatano katika mji wa Ramallah.

Oman kwa muda mrefu imekuwa ikifahamika Mashariki ya Kati kuwa haina upande kama vile Switzerland ilivyo kwa diplomasia ya kimataifa. Nchi hiyo imesaidia kusimamia kwa siri mazungumzo kati ya Marekani na Iran mwaka 2013 ambayo yalipelekea makubaliano ya kihisitoria ya mkataba wa nyuklia uliosainiwa Geneva miaka miwili baadae.

Imekuwa ikitoa ushauri kusaidia Israel na Wapalestina wakutane japokuwa haifanyi hivyo kama msuluhishi wa moja kwa moja.

Mwaka 2018, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alifanya ziara ambayo ni nadra kutokea mjini Muscat na kujadili juhudi za amani Mashariki ya Kati na kiongozi wa Oman Sultani Qaboos.

XS
SM
MD
LG