Akizungumza katika sherehe ya kumkaribisha katika Uwanja wa Ndege wa Ben-Gurion huko Tel Avivi, Trump amesema fursa hiyo inatoa nafasi ya kuutokomeza ugaidi na inaweza kuleta mafanikio kwa ‘Kushirikiana pamoja.”
Amewasili katika safari ya kihistoria ambapo ndege yake iliruka moja kwa moja kutoka Saudi Arabia mpaka Israeli baada ya kutoa hotuba yake Jumapili Riyadh juu ya umuhimu wa kuungana pamoja katika kupambana na ugaidi.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alinukuu hotuba ya Trump katika salamu zake za kumkaribisha, akisema Israeli ina azma ileile ya kufikia amani na imekunjua mikono yake kufikisha amani kwa majirani zake wote, ikiwemo Palestina.”
Trump ameonyesha hamu yake yakuanzisha mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestina ambayo yalivurugika mwaka 2014.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema kuwaambia waandishi wanaosafiri na rais kwamba Trump “anahisi kuna fursa kwa kipindi hiki kuendeleza mchakato huo.
“Nafikiri rais ameonyesha nia kutumia juhudi zake binafsi katika suala hili , iwapo tu uongozi wa Israeli na Palestina watakuwa tayari kufanya hima ya kutafuta suluhu hiyo,” amesema Tillerson.