Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:04

"Trump ana njia chache kudhibiti programu ya nyuklia ya Korea Kaskazini"


Watu Korea Kusini wanaangalia kurushwa kwa kombora la kati kulikofanywa na Korea Kaskazini hivi karibuni.
Watu Korea Kusini wanaangalia kurushwa kwa kombora la kati kulikofanywa na Korea Kaskazini hivi karibuni.

Katika jumla ya hiari zilizokuwepo kwa Marekani ni kuishambulia, au kukubaliana au kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini.

Mambo haya pengine pekee yanaweza kuizuia Korea Kaskazini kuendelea kutengeneza kombora la balistika lenye nyuklia linaloweza kufika katika mabara mbali mbali duniani (ICBM).

Na pengine njia mbadala pekee ambayo inaweza kuwa na mafanikio kwa kiasi fulani ni kufuata utaratibu wa makubaliano kama yale yalifanywa mwaka 2015 kwa mwafaka wa Nyuklia ya Iran ambao uliitwa “ni makubaliano mbovu kuliko yote”na Rais wa Marekani Donald Trump.

Haya ni baadhi ya maono na mapendekezo yaliyotolewa na mtaalamu wa kuzuia kusambaa kwa silaha kali Robert Litwak wakati wa mazungumzo aliyoyafanya kwenye mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya East Asia huko Seoul kuhusu kitabu chake kinachoitwa :Jinsi ya kuzuia program ya nyuklia ya Korea Kaskazini isienee.

Litwak ni mkurugenzi wa tafiti za usalama za kimataifa katika Kituo cha Woodrow Wilson kwa ajili ya wanazuoni na amewahi kutumikia nafasi ya ukurugenzi wa kuzuia kuenea kwa silaha za maangamivu chini ya utawala wa Rais mstaafu Bill Clinton.

Marekani haiwezi kuendelea kusubiri serikali kandamizi ya Korea Kaskazini kuporomoka kwa shinikizo la vikwazo vya kimataifa. Litwak amedadisi kuwa badala yake ni lazima papatikane makubaliano ya uhalisia ambayo yataiwezesha Pyongyang kuendelea kuweka programu yake ya nyuklia na makombora ya balistika kwa kubadilishana na kusimamisha majaribio na uundaji wa silaha hizo zaidi.

“Simulizi litakuwa kwamba Marekani haitaki Korea Kaskazini iwe ni taifa lenye silaha za Nyuklia lakini hii kwa namna fulani itakuwa ni hatua ya mpito, kusimamisha uwezo wake katika lengo la muda mrefu la kuondoa silaha za maangamivu katika Rasi ya Korea,” amesema mtaalamu huyo.

Juhudi za hivi sasa za mataifa makubwa kuwawekea vikwazo vya kimataifa, kuwatenga kidiplomasia na kuwazuia kijeshi umeshindikana kusitisha au kupunguza kasi ya Korea Kaskazini katika kutengeneza silaha hizo, Litwak amesema.

Jaribio la kombora la masafa ya kati iliofanywa na Pyongyang Jumapili inaonyesha kusaidia hoja hii iliyotolewa na mtaalamu huyu. Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini (KCNA) limesema jumatatu kuwa mafuta yaliotumika kurusha kombora hilo yamewezesha kufikia umbali wa kilometa 500 na kupaa juu kwa mnyanyuko wa kilometa 560, na kuthibitisha kuwa inaonyesha upo uwezekano wa mfumo huu hivi karibuni kuweza kuchukua kichwa chenye silaha ya nyuklia na kukifikisha kwenye eneo lililokusudiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema jaribio hilo la Kombora “halikubaliki” na “linaleta wasiwasi” katika mahojiano yake na Fox News.

Lakini hata hivyo amesema kutakuwepo na ongezeko la shinikizo la vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia kuilazimisha serikali ya Kim Jong Un kubadilisha mwenendo wake.

Litwak ametoa hoja kuwa China na Korea Kaskazini ambao ni washirika wakuu katika biashara, wamekuwa “wakikinzana katika mikakati inayohusu maslahi ya Rasi ya Korea.”

Beijing inataka kuhakikisha hakuna silaha za maangamivu nchini Korea Kaskazini, lakini inaendelea kuonyesha hairidhishwi na vikwazo wakati ikiendelea kuhakikisha utulivu wa eneo hilo la rasi na kuisaidia serikali ya Kim ilikuepusha nguvu za kijeshi za Marekani na Korea Kusini kuenea katika eneo hilo.

Kwa upande wake Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kuwa wakati anapinga programu ya nyuklia ya Korea Kaskazini, “vitisho vyovyote dhidi ya Korea Kaskazini havikubaliki.”

Hivi karibuni Moscow ilianzisha safari ya ferry kati yake na Korea Kaskazini na kupuuza pingamizi lililotolewa na Washington.

XS
SM
MD
LG