Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:20

Trump kufanya 'kila awezacho' kuleta amani Mashariki ya Kati


Rais Donald Trump na Rais Mahmoud Abbas katika mkutano wa pamoja huko Bethlehem, Mei 23, 2017.
Rais Donald Trump na Rais Mahmoud Abbas katika mkutano wa pamoja huko Bethlehem, Mei 23, 2017.

Rais Donald Trump Jumanne ameahidi kufanya “kila atachoweza” kuleta amani Mashariki ya Kati, akirejea matarajio ya viongozi waliomtangulia ambao walijaribu na kushindwa kufikia lengo hilo.

Juhudi zake katika kusimamia amani zimekuja mapema wakati uongozi wa Trump umefunikwa na mgogoro wa kisiasa, sehemu ya matatizo hayo yakiwa yamesababishwa na kauli za rais mwenyewe.

“Ninamatumaini ya kweli kuwa Marekani inaweza kuwasaidia Waisraeli na Wapalestina kufikia amani na kuleta matumaini mapya katika eneo la Mashariki ya Kati na watu wake,” Trump amesema baada ya mkutano wake wa saa nzima huko Bethlehem na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas.

Trump aliongeza kuwa anaimani kuwa “ Iwapo Israeli na Palestina zitafikia amani, itawezesha kuanzisha mchakato wa amani Mashariki ya Kati yote, na hilo litaleta mafanikio makubwa.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Trump, Abbas amesema tatizo la msingi kwa upande wa watu wa Palestina ni kuhusu uvamizi wa Israeli na ujenzi wa makazi yao, na kitendo cha Israeli kutotaka kuitambau Palestina.

“Tatizo sio Uyahudi bali ni uvamizi,” ameongeza kusema Abbas.

Abbas amesisitiza kuwa yuko tayari kukubali suluhisho la kuwepo mataifa mawili na mipaka iliyowekwa mwaka 1967.

XS
SM
MD
LG