Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:13

Baraza la Maulamaa lataka bidhaa za Marekani, Israel kususiwa Indonesia


Waandamanaji wa Kiislam wakilaani uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.
Waandamanaji wa Kiislam wakilaani uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Maelfu ya Waislam walijitokeza kuandamana kutoka katika msikiti mkubwa wa mjii mkuu wa Indonesia katika makutano ya barabara huko Jakarta Jumapili, kupinga uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Yalikuwa maandamano makubwa kuliko yote Indonesia tangu Trump kutangaza hatua yake ya utata mapema mwezi Disemba kubadilisha sera ya Marekani iliyodumu kwa miongo mingi.

“Tunahimiza nchi zote kukataa hatua hiyo binafsi na uamuzi huo kinyume cha sheria wa Rais Donald Trump kuifanya Jerusalem ni mji mkuu wa Israel,” Anwar Abbas, katibu mkuu wa Baraza la Maulama nchini Indonesia aliwaeleza halaiki kubwa ya watu.

“Tunatoa wito kwa watu wote wa Indonesia kususia bidhaa za Marekani na Israel katika nchi yetu,” iwapo Trump hatositisha uamuzi wake, Abbas amesema, akisoma kutoka katika ombi rasmi ambalo litakabidhiwa kwa balozi wa Marekani nchini Indonesia.

Wengi wa waandamanaji walikuwa wamevaa vitambaa vyeupe na wakipeperusha bendera za Palestina na kubeba mabango, baadhi yake yakisomeka: “Amani, upendo, na uhuru wa Palestina.”

Polisi wanakadiria kuwa watu walioshiriki katika maandamano hayo, yaliyoandaliwa na vikundi mbalimbali vya Kiislam, walikuwa 80,000.

Maandamano hayo yalifanyika kwa amani, lakini mistari ya maaskari waliosimama mbele ya uzio wa eneo la ubalozi wa Marekani, mjini Jakata kuzuia makundi ya watu kutofikia eneo hilo. Msemaji wa polisi ameeleza askari 20,000 na wanajeshi waliwekwa katika eneo hilo kuhakikisha kuna usalama.

Kumekuwepo na mlolongo wa maandamano nchini Indonesia juu ya suala la Jerusalem, yakiwemo yale ambayo waandamanaji wenye msimamo mkali waliunguza bendera za Marekani na Israeli.

Umuhimu wa Jerusalem, mji mtakatifu wa Wayahudi, Waislam na Wakiristo, ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyozuia kupatikana amani ya kudumu kati ya Israeli na Palestina.

Eneo la Jerusalem ya mashariki ilitekwa na Israel katika vita ya mwaka 1967 na kukaliwa kwa mabavu hatua ambayo haitambuliwi kimataifa.

XS
SM
MD
LG