Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:13

Trump anatarajiwa kuitambua Jerusalem


Sehemu ya mji wa Jerusalem, Israeli
Sehemu ya mji wa Jerusalem, Israeli

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kuitambua rasmi mapema wiki ijayo Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel, kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini Marekani.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa Trump hatatangaza uamuzi wa mwisho wa kuhamisha Ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv wakati akiutambua mji huo kuwa makao makuu.

Tayari kuna hali ya utata wakati pande zote mbili za Israeli na Palestina zikiendelea kudai kuwa Jerusalem ni mji wao mkuu.

Wakati wa kampeni za urais Trump aliahidi kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

Hakuna taarifa zilizoeleza iwapo Trump ataelezea kama Jerusalem ni sehemu ya mji mkuu au ni mji mkuu wenyewe kamili—moja kati ya vitu vyenye ukakasi mkubwa katika mahusiano ya Israeli na Palestina kufuatia mgogoro wao ambao wameachiwa wao wenyewe kufikia makubaliano ya mwisho.

Hiyo itakuwa hatua ambayo haijawahi kutokea ambapo maafisa wa serikali ya Palestina tayari wametahadharisha kuwa itadhoofisha mchakato mzima wa mazungumzo ambayo yanaendelea.

Uongozi wa Trump unapanga kutoa pendekezo kwa urefu la kufikia amani pande hizo mbili katika miezi ijayo.

Jared Kushner, mkwe wake Trump na mshauri mkuu wa uongozi huo katika juhudi za kutafuta amani, atazungumza juu ya mpango huo katika safu ya taasisi ya Brookings Institution wakati wa wikiendi.

XS
SM
MD
LG