Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 12:59

Kombe la Dunia: Nchi za Afrika katika makundi tofauti


Wachezaji wa zamani Diego Maradona na Cafu katika ratiba ya kombe la dunia, Moscow
Wachezaji wa zamani Diego Maradona na Cafu katika ratiba ya kombe la dunia, Moscow

Nchi za Afrika zitakazoshiriki katika fainali za kombe la dunia nchini Russia hapo mwakani zitakuwa katika makundi tofauti katika hatua ya mwanzo ya michuano, hali ambayo inaongeza uwezekano wa nchi ya Afrika kuingia katika raundi ya pili.

Ratiba iliyofanyika mjini Moscow Ijumaa imezigawa nchi 32 katika fainali hiyo kwenye makundi manane. Nigeria na Morocco zinaonekana kuwa katika makundi magumu zaidi kuliko nchi nyingine za Afrika.

Nigeria ipo katika kundi D ambalo linaweza kuchukuliwa kama kundi gumu zaidi likiwa na Croatia, Iceland na mabingwa wa zamani Argentina. Morocco ipo katika kundi B pamoja na Spain, Ureno na Iran.

Misri pia ipo katika wakati mgumu kwa kuwa katika kundi A ambalo lina wenyeji Russia, Uruguay na Saudi Arabia. Senegal ipo kundi H ambapo itapambana na Poland, Colombia na Japan, wakati Tunisia itakuwa katika kundi G lenye timu za Uingereza, Ubelgiji na Panama.

Mabingwa watetezi Ujerumani wako katika kundi F lenye timu za Mexico, Sweden, na South Korea wakati Brazil - siku zote wanapewa nafasi ya kuchukua kombe hilo - wapo katika kundi E lenye timu za Switzerland, Costa Rica na Serbia.

Fainali za kombe la dunia 2018 zitaanza Juni 14 na kuchukua mwezi mzima hadi Julai 15. Jumla ya mechi 64 zitachezwa katika viwanja 12 vilivyo katika miji 11 tofauti nchini Russia. Wenyeji Russia watafungua dimba na Saudi Arabia katika mechi ya kwanza kwenye uwanja wa Luzhniki, Moscow.

Misri na Morocco zitakuwa nchi za kwanza za Afrika kujimwaga uwanjani Juni 15, Misri ikipambana na Uruguay katika mechi za kundi A, wakati Morocco itagongana na Iran katika mechi za kundi B siku hiyo hiyo ya Juni 15.

Makundi kamili ya Kombe la Dunia 2018

Kundi A: Russia, Saudi Arabia, Misri, Uruguay

Kundi B: Ureno, Spain, Morocco, Iran

Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark

Kundi D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria

Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia

Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden, South Korea

Group G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, Uingereza

Group H: Poland, Senegal, Colombia, Japan

XS
SM
MD
LG