Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 08:07

Mwanasiasa mkongwe wa Palestina Saeb Erekat afariki kutokana na Covid-19


Mwanasiasa mkongwe wa kutetea uhuru na haki za Wapalestina Saeb Erekat aliyeaga dunia tarehe 10 Novemba 2020.
Mwanasiasa mkongwe wa kutetea uhuru na haki za Wapalestina Saeb Erekat aliyeaga dunia tarehe 10 Novemba 2020.

Mwanasiasa mkongwe wa Palestina aliyesimamia mazungumzo ya kutafuta suluhuhiso kwa mzozo kati ya Palestina na Israel, Saeb Erekat, amefariki dunia Jumanne akiwa na umri wa miaka 65, wiki kadha baada ya kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa covid 19.

Rais wa Palestina Mahmud Abbas alisema katika taarifa kwamba “kuondoka kwa ndugu,rRafiki na shujaa DktSaeb Erekat ni hasara kubwa kwa Palestina na wanainchi wetu. Tumehuzunika sana.”

Erekat, msomi na mwandishi wa vitabu alishiriki katika mazungumzo yote na Israeli tangu mwaka wa 1991.

Alipigania kwa muda mrefu kupatikana suluhu la kuwepo mataifa mawili huru, Palestina na Israel.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG