Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:30

Hali ya mvutano yaongezeka mashariki ya Jerusalem


Afisa wa polisi wa Israel akimshikilia mwanadamanaji wa Palestina wakati wa maadamano kabla ya Mahakama kutoa uamuzi wa kuchukuliwa makazi ya familia ya Wapalestina, huko eneo la Sheikh Jarrah, jirani na mashariki ya Jerusalem, Mei 5, 2021.
Afisa wa polisi wa Israel akimshikilia mwanadamanaji wa Palestina wakati wa maadamano kabla ya Mahakama kutoa uamuzi wa kuchukuliwa makazi ya familia ya Wapalestina, huko eneo la Sheikh Jarrah, jirani na mashariki ya Jerusalem, Mei 5, 2021.

Hali ya mvutano imeongezeka Jumapili huko mashariki mwa Jerusalem inayokaliwa na Israeli baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa wakati wa mapambano kati ya waandamanaji na polisi kwenye uwanja wa mskiti wa al Aqsa.

Ghasia kwenye msikiti huo mtakatifu na maeneo ya mji wa kale wa Jerusalem, zimechochewa na juhudi za miaka mingi za walowezi wakiyahudi kutaka kuchukua nyumba za wapalestina huko mashariki ya Jerusalem na zimezusha wasiwasi duniani kote.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imeitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo kesho Jumatatu kujadili kuongezeka ghasia zinazotokea wakati wa usiku.

Wajumbe wa kamati inayotetea Wapalestina kurudi kwenye makazi yao ya kijadi, High Committee of Return Marches imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za dhati dhidi ya Israeli kutokana na ghasia hizo.

Akizungumza kabla ya mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba Israel itachukua hatua thabiti kutangaza sheria za kurudisha utulivu Jerusalem huku ikiheshimu haki za kuabudu za dini zote.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Karibu Wapalestina 121 walijeruhiwa wakati wa mapambano ya Jumamosi usku kuamkia Jumapili wengi kutokana na risasi za mpira kulingana na shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina.

Mataifa ya Kiarabu pamoja na yale manne yaliyorudisha uhusiano na Israel hivi karibuni, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Morocco na Sudan yamelaani hatua za Israel kwenye msikiti wa Al-Aqsa na yana unga mkono malalamiko ya wa Palestina.

XS
SM
MD
LG