Israeli iliipiga Gaza City kwa mashambulizi ya anga Jumatatu, na kumuua kamanda mwandamizi wa wanamgambo wa Palestina, nao wanamgambo wa Palestina walifanya mashambulizi ya roketi dhidi kwa Israeli wakati ghasia katika eneo hilo zilipoingia wiki ya pili.
Tangu mapigano yalipoanza Mei 10, Wapalestina wasiopungua 200 wameuawa, wakiwemo watoto wasiopungua 59 na wanawake 35, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza. Waisraeli wasiopungua 10 wameuawa katika mashambulizi ya roketi, pamoja na mtoto wa miaka 6.
Jeshi la Israeli lilisema liliharibu mahandaki ya kilomita zipatazo 15 huko Gaza yaliyotumiwa na Hamas, pamoja na jengo la orofa tano ambalo lilikuwa na wizara ya Maswala ya Kidini inayoendeshwa na Hamas, na kumuua kamanda wa Jihad wa Kiislam wa kaskazini mwa Gaza, Hussam Abu Harbeed.
Ikijibu mashambulizi, kundi la Jihad lilifyatua roketi katika mji wa pwani wa Israel wa Ashdod na watu saba wamejeruhiwa kwa mujibu wa maafisa.