Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:35

Israeli yaendelea na mashambulizi ya anga Gaza City


Wazima moto Wapalestina wakijitahidi kuuzima moto katika kiwanda cha magodoro baada ya kupigwa na mabomu yaliyorushwa na kikosi cha mizinga cha Israeli huko Gaza Mei 17, 2021.REUTERS/Ashraf Abu Amrah
Wazima moto Wapalestina wakijitahidi kuuzima moto katika kiwanda cha magodoro baada ya kupigwa na mabomu yaliyorushwa na kikosi cha mizinga cha Israeli huko Gaza Mei 17, 2021.REUTERS/Ashraf Abu Amrah

Israeli mapema Jumatatu imefanya mashambulizi ya anga huko Gaza City wakati ghasia katika eneo hilo zimeingia wiki ya pili.

Jeshi la Israeli linasema wamelenga mahandaki yanayotumiwa na kundi la Hamas na makazi ya makamanda kadhaa wa kundi hilo linalotawala Gaza.

Shambulizi la leo limefuatia matamshi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ambaye Jumapili amesema hana mpango wowote wa kusitisha mara moja mashambulizi mabaya ya anga huko Gaza.

Alizungumza jana wakati ndege za jeshi la Israeli ziliposhamabulia na kuharibu majengo matatu na kuuwa watu 42.

Jumapili asubuhi, Hamas ilirusha roketi kutoka maeneo ya raia huko Gaza kuelekea maeneo ya raia wa Israel.

Tangu mapigano kuanza tarehe 10 Mei, Wapalestina 197 wameuawa wakiwemo watoto 58 na wanawake 34, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina. WaIsrael 10 nao wameuwawa katika mashambulizi ya roketi.

XS
SM
MD
LG