Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:29

Sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina laonyesha matumaini kudumu


Mwanamke wa Kipalestina aliyerejea katika makazi yake yaliyopigwa bomu na Israeli akipika chakula, baada ya kusitishwa mapigano kati ya Israeli na Hamas yaliyosimamiwa na Misri (Photo by MOHAMMED ABED / AFP)
Mwanamke wa Kipalestina aliyerejea katika makazi yake yaliyopigwa bomu na Israeli akipika chakula, baada ya kusitishwa mapigano kati ya Israeli na Hamas yaliyosimamiwa na Misri (Photo by MOHAMMED ABED / AFP)

Wakati sitisho la mapigano tete kati ya Israeli na wanamgambo wa Palestina llilianza Jumamosi baada ya siku 11 za mapigano, Wapatanishi kutoka Misri wamefanya mazungumzo na pande zote hasimu ili kuimarisha sitisho hilo.

Ujumbe wa Misri umewasili Israeli Ijumaa na tangu ulipowasili umekuwa ukisafiri kati ya maeneo ya Israeli na Palestina, mwanadiplomasia wa Misri na maafisa wa Hamas wamesema Jumamosi.

Mwanadiplomasia wa Misri amesema mazungumzo ya kuhakikisha kupata sitisho la muda mrefu kumaliza ghasia ni pamoja na kubuni hatua za kuzuia vitendo vilivyopelekea ghasia hizo.

Serikali ya Misri imesema imepeleka msafara wa malori 130 ya vifaa vya afya vinavyiohitajika kwa haraka sana na aina nyengine za misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, misaada hiyo inatarajiwa kuwasili Jumamosi.

Jumamosi ilikuwa siku ya kwanza kamili ya sitisho la mapigano ambalo limemaliza mvutano mkubwa wa n ne kati ya Israel na Kikundi cha wanamgambo wa Hamas kwa kipindi cha zaidi ya muongo moja.

Israel na Hamas wote wamedai ushindi siku ya Ijumaa.

Mtoto akifurahia kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza
Mtoto akifurahia kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameandika katika Twitter Ijumaa kuwa “atasafiri kwenda Mashariki ya Kati katika siku zijazo” na kukutana na viongozi wa Israeli, Palestina na wengineo katika eneo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Alhamisi kuwa Blinken atazungumzia juhudi za kusaidia na kufanya kazi pamoja kujenga mustakbali uliobora kwa Israeli na Palestina” wakati wa ziara yake.

Viongozi wa dunia wamepongeza suluhu inayosimamiwa na Misri.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Dominic Raab amesema katika Twitter, “Pande zote lazima zishirikiane kudumisha sitisho na kumaliza wimbi la ghasia zisizo kubalika na vifo vya raia.

EU foreign policy chief Josep Borrell said in a statement that working toward a "two-state solution" was the only viable option.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema katika taarifa yake kuwa kushirikiana ili kufikia suluhu ya kuwepo mataifa mawili ndio njia bora pekee.

XS
SM
MD
LG