Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:29

Wademokrat watoa wito wa kusitishwa vita kati ya Israeli na Palestina


Seneta Chris Murphy
Seneta Chris Murphy

Kukiwa hakuna dalili za vita kati ya Israeli na Palestina kumalizika hivi karibuni huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea, Wademokrat kwenye Bunge la Marekani wanatoa wito wa kusitishwa mapigano.

Nao wabunge wa Chama Cha Republican wanalaani mashambulizi ya Hamas wakisema huwezi kulinganisha kwa usawa vitendo vya pande hizo mbili.

Ghasia zinazoendelea kati ya Wapalestina na Israel

Kundi la Hamas kwa siku 10 mfululizo limekuwa likifyatua roketi ndani ya Israel katika kile wapiganaji wake wanasema ni ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya Wapalestina, huku Israel ikijibu kwa mashambulio ya anga kwenye ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israeli likishamblia eneo la Ukanda wa Gaza, Jumatano, Mei 19, 2021. (AP Photo/Tsafrir Abayov)
Jeshi la Israeli likishamblia eneo la Ukanda wa Gaza, Jumatano, Mei 19, 2021. (AP Photo/Tsafrir Abayov)

Chris Murphy Seneta Mdemokrat anasema Israeli ilifanya makoso kuendelea na mpangio wa kujenga makazi na kuwaondowa Wapalestina ikiwa ni kama njia ya makusudi ya kuhujumu taifa la baadae la Palestina.

Seneta Murphy anaeleza : "Sera hizi huenda zikasaidia kuunganisha pamoja Netanyahu na muungano wake wa kisiasa, lakini zimesaidia kuchochea hali ya kutokuwa na matumaini miongoni mwa Wapalestina na mustakbali wao. Uongozi wa Wapalestina ulifanya pia makoso kwa kueneza Wazi chuki dhidi ya Israeli kama msingi wake wa kubaki madarakani."

Roketi zinarushwa na kikundi cha Hamas kuelekea Israeli kutoka Gaza City, eneo linalodhibitiwa na kundi la Palestina la Hamas, Mei 11, 2021
Roketi zinarushwa na kikundi cha Hamas kuelekea Israeli kutoka Gaza City, eneo linalodhibitiwa na kundi la Palestina la Hamas, Mei 11, 2021

Msimamo wa Wademokrat Kuhusu Mageuzi

Wademokrats wanaopendelea mageuzi, wenye msimamo mkali wa kushoto akiwemu Seneta Bernie Sanders na Mbunge Alexandria Ocasio Cortez wanatoa wito kutathmini upya msaada wa Marekani kwa Israel kwa sababu ya majeruhi ya kiraia yanayosababishwa na mashambulio ya anga ya Israel.

Seneta Bernie Sanders
Seneta Bernie Sanders

Lakini wabunge wengi wenye msimamo wa wastani wanatoa wito wa kusitishwa mapigano. Seneta Bob Menendez Mdemokrat anasema juhudi za kidiplomasia zinaendelea.

Seneta Menendez : Wote waziri Blinken na rais binafsi wanajihusisha kikamilifu katika juhudi za kidiplomasia za chini kwa chini, za moja kwa moja na serikali ya Israel na Misri pamoja na washirika wengine katika kanda hiyo ili kuweza kukomesha mapigano hayo.

Warepublican kwa upande wao wanasema huwezi kulinganisha wajibu wa pande zote mbili. Seneta wa walio wachache kwenye baraza la Seneta Mitch McConnell anahisi Wademokrat wanawalaumu Waisrael hivi sasa.

McConnel awashutumu Wademokrat

Seneta Mitch McConnell
Seneta Mitch McConnell

McConnell aeleza : Kuna idadi kubwa ya Wademokrat wanataka kuwalaumu Waisrael na kujifanya kuna usawa wa majukumu. Hakuna usawa wa kimaadili, kundi la kigaidi upande mmoja linalowatumia kwa hakika Wapalestina kwa faida zao binafsi kwa kuwaweka hatarini mara kwa mara, na huku Waisraeli wakilenga shabaha zao ili kulinda nchi yao.

Wito wa Warepublikan

Masemeta Warepublican wanatoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi kuilinda Israeli, kwa kuongeza msaada wake wa kijeshi wakati wakilaani hatua ya utawala wa Biden kujiunga na mkataba wa Nyuklia na Iran.

Na wakati huo huo utawala wa Biden ukikabiliwa na changamoto kutoka Wademokrat wapenda mageuzi wanaotaka kuzuia biashara ya silaha yenye thamani ya dola milioni 735 kwa Israel. Muda wa kukamilisha mkataba huo umeshakaribia, hakuna dalili za kuweza kuuzia kutekelezwa.

XS
SM
MD
LG