Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:38

Jeshi la Msumbiji laukomboa mji wa Palma


Kambi ya wakimbizi huko Metuge, ambapo watu waliokimbia makazi yao kutoka Cabo Delgado, Msumbiji wanaishi. Picha imepigwa Machi 27, 2021.
Kambi ya wakimbizi huko Metuge, ambapo watu waliokimbia makazi yao kutoka Cabo Delgado, Msumbiji wanaishi. Picha imepigwa Machi 27, 2021.

Jeshi la Msumbiji linasema linaendelea kuukomboa mji wa kaskazini wa Palma wenye kituo cha gesi, ambao ulitekwa na wapiganaji wa Kiislam wenye mahusiano na kikundi cha Islamic State mwezi Machi, likidai idadi kubwa ya wapiganaji walikuwa wameuawa katika mapigano hayo.

Palma ulitekwa katika shambulizi lililopangwa hapo Machi 24, ikiwa kusambaa kwa uasi ambao umeendelea kupamba moto katika Jimbo la Cabo Delgado kwa zaidi ya miaka mitatu.

Jumapili, Jeshi hilo liliwasindikiza maafisa na waandishi wa habari kwenda mjini Palma.

Kamanda Chongo Vidigal, kiongozi wa operesheni za kijeshi za kuukomboa mji wa Palma, ameiambia televisheni ya serikali TVM kuwa eneo hilo hivi sasa liko “salama”, licha ya kusita kutangaza kuwa jeshi limepata udhibiti kamili wa mji huo.

“Eneo la uwanja wa ndege ni sehemu pekee tuliyohitaji kulidhibiti na tulifanya hivyo asubuhi ya leo. Ni sehemu salama kabisa,” Vidigal alisema.

Wanajeshi wakilinda doria huko Carbo Delgado.
Wanajeshi wakilinda doria huko Carbo Delgado.

“Nafikiri kuwa ni idadi kubwa ya magaidi waliouawa,” amesema, akiongeza kuwa mamlaka zitatoa idadi kamili baadae.

Maelfu wameukimbia mji huo wenye wakazi 75,000 ambapo darzeni ya raia waliuawa, kulingana na idadi iliyotolewa na serikali hapo awali, na kampuni kubwa ya nishati ya Total imeondoka katika eneo ambapo mradi wa gasi uliogharimu mabilioni ya dola unaendelezwa.

Picha za video zilionyesha wanajeshi wakifunua maiti kutoka kwenye mifuko ya plastiki katika mitaa hiyo.

Picha nyingine zilionyesha mabaki ya majengo yalioungua, ikiwemo mabenki, hospitali na ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali.

XS
SM
MD
LG