Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:17

Ureno kuisaida Msumbiji kupambana na wanamgambo wenye siasa kali

(FILES) Machi 07, 2018 wanajeshi wa Msumbiji wakifanya doria katika mitaa baada ya serikali kuongeza ulinzi baada ya siku mbili za mashambulizi yaliyofanywa na kikundi cha Waislam wenye siasa kali mwezi Oktoba 2017 katika eneo la Mocimboa da Praia, Mozambique. -…

Ureno inasema itaisaidia Msumbiji katika masuala ya uchukuzi na kuimarisha uwezo wake wa kijeshi.

Msaada huo wa kijeshi utaiwezesha Msumbiji kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali wanaotishia usalama kwenye jimbo la kaskazini lenye utajiri wa mafuta la Cabo Delgado.

Waziri wa Ulinzi wa Ureno Joao Gomes Cravinho akimaliza ziara ya siku tatu nchini humo amesema tume ya maafisa wa jeshi wa ureno wataanza kufanya kazi kuanzia mwezi ujao na wenzao wa msumbiji juu ya mipango hiyo.

Anasema Ureno inayochukua uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya mwakani itahimiza utekelezaji wa ombi la msaada la Msumbiji lililokuwa tayari limewasilishwa Brussels.

Kulingana na shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu, ghasia katika jimbo la Cabo Delgado zimesababisha mzozo wa kibinadamu ambapo watu 2,000 wanaripotiwa wameuliwa na zaidi ya nusu milioni kupoteza makazi yao.

XS
SM
MD
LG