Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:51

Askofu ailamu jumuiya ya kimataifa kwa kukaa kimya juu ya mgogoro wa Msumbiji


Wanawake wakitayarisha hifadhi ya chakula huko, Cabo Delgado, Msumbiji
Wanawake wakitayarisha hifadhi ya chakula huko, Cabo Delgado, Msumbiji

Mashambulizi katika jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Cabo Delgado, yanaendelea kusababisha watu kukimbia makazi yao, huku serikali ikionekana kushindwa kukabiliana na mashambulizi hayo yanayofanywa na wapiganaji wenye misimamo mikali wa kundi la Kiislam.

Askofu wa Pemba mji mkuu wa jimbo hilo, analaani jinsi jumuia ya kimataifa ilivyo kaa kimya kutokana na machafuko hayo.

Mashambulio hayo yalioanza tangu 2017 katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa gesi kaskazini mwa Msumbiji yanaripotiwa kuongezeka mnamo mieizi michache iliyopita. Kijiji cha Macomia ni mojawapo ya vijiji vilivyoshambuliwa hivi karibuni.

Kufuatana na asasi isiyo ya kiserkali ya ACLED karibu watu elfu moja mia moja wameuliwa tangu wanamgambo wenye itikali kali kuanzisha kampeni yao ya mashambulizi. Na maelfu wamelazimika kukimbia makazi yao wengi wao wakikimbilia mjini Pemba.

Askofu wa Kanisa la Katoliki mjini Pemba Luis Fernando Lisboa amekupaza sauti kulaani hali ilivyo na kutahadharisha juu ya maafa yanayo sababishwa na vita hivyo.

Askofu Luiz Fernando : "Hatuwezi kuwachukulia watu kuwa ni takwimu tu. Ni binadamu na kila binadamu anakuwa na hadithi , kuna msongo wa akili kutokana na vita. Huenda inatokana na kupoteza makazi yao au kwa sababu wamewaona jamaa wa familia zao wakiuliwa au huenda jamaa zao hawajulikani walipo.

Wachambuzi nchini Msumbiji wanailaumu serikali ya Rais Filipe Nyusi kwa kutoshughulikia vilivyo tatizo hilo la kaskazini mwa nchi yake.

Mwezi Mei jeshi la Taifa liliripoti kuwauwa wapiganaji 50 katika mapigano mawili tofauti katika jimbo hilo la kaskazini ambako wapiganaji wamefanya mashambulizi 11 mwaka 2020 pekee.

Askofu Lisbo akizungumza na shirika la habai la Lusa, anasema tumezowea vita, huko Iraq na Syria na sasa kuna vita huko Msumbiji lakini bado hawajaona masnada unaohitajika kutoka nje.

Askofu anasema : "Watu wengi wamefadhaika, na hivyo hatuwezi kutegemea kuwapatia chakula pekee yake, ni jambo dogo tu. Chakula ni muhimu kweli, inakuwezesha kuendelea kuishi lakini baadhi ya watu wamefadhaika sana kutokana a madhila yanayowakumba. Kwa hivyo tunashuhudia matatizo ya kiakili na hivyo kunahitajika msaada wa kijamii.

Kundi la Ahlu Sunna wal-Jamaa linalodhaniwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State limedai kuhusika na mashambulizi na katika siku za hivi karibuni machafuko yameongezeka huko Cabo Delgado na kuzusha matatizo makubwa kwa serikali na makampuni ya kigeni yaliyowekeza mabilioni ya dola katika mradi wa gesi inayopatikana katika bahari ya Hindi. Makampuni ya Exxon Mobil na Total hivi sasa ndio yanaendesha mradi wa kutengeneza kiwanda kikubwa kugeuza gesi kuwa maji maji kwa urahisi wa kusafirisha bidhaa hiyo nje.

XS
SM
MD
LG