Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:59

Papa Francis apokewa kwa shangwe kubwa Msumbiji


Papa Francis alipokuwa anaondoka Rome kuelekea Maputo, Msumbiji Septemba 4, 2019.
Papa Francis alipokuwa anaondoka Rome kuelekea Maputo, Msumbiji Septemba 4, 2019.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Francis amepokelewa na maelfu ya wananchi wa Msumbiji Jumatano – akiwemo Rais Filipe Nyusi – wakati akianza ziara yake ya kwanza tangu awe papa katika nchi hiyo iliyoko kusini mwa Afrika.

Papa aliwasili Jumatano usiku uwanja wa ndege wa Maputo huku kundi kubwa la watu likimshangilia. Wanawake wengi walivalia sare ya vazi la asili la Msumbiji likiwa na picha za kuvutia za Francis.

Katika ujumbe aliorikodi uliotolewa kabla ya kuwasili kwake, Papa aliwahutubia wananchi wa Msumbiji katika lugha inayozungumzwa zaidi nchini humo Kireno.

“Ninawakaribisha nyote mje katika maombi yangu ili Mungu, Muumba wa kila kitu, aimarishe maelewano, undugu nchini Msumbiji na Afrika nzima, ikiwa ni fursa pekee ya kuwepo amani thabiti na ya kudumu.

Ziara ya papa nchini Mozambique inafanyika wakati makubaliano ya amani hivi karibuni yalipofikiwa yanayo kusudia kumaliza miongo kadhaa ya uvunjifu wa amani baada ya vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Chama tawala cha Frelimo na Chama cha Upinzani Renamo.

Katika ziara yake ya siku tatu, papa atakutana na wabunge, vijana na viongozi wa dini, na kutoa hotuba tatu Alhamisi kabla ya kuongoza ibada ya pamoja siku ya Ijumaa.

Baada ya kumaliza ziara yake Msumbiji, Francis ataendelea na ziara yake katika visiwa vya Madagascar na Mauritius, ambako pia alipeleka mapema ujumbe wake kupitia picha za video.

Papa katika hotuba hiyo aliongea KItaliano kwa watu wa Mauritius, ambao wanaongea pia Kiingereza, Kifaransa, Creole na Kihindu na kwa watu wa Malagasy, wanao ongea Kifaransa na Kimalagasy.

XS
SM
MD
LG