Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:10

Papa Francis awataka Wakristo na Waislamu kuishi kwa amani


Papa Francis akiwasili Cairo
Papa Francis akiwasili Cairo

Papa Francis ameanza ziara ya siku mbili nchini Misri, ambapo atakuwa akihubiri amani kati ya Wakristo na Waislamu nchini humo kufuatia shambulizi la bomu katika kanisa la Coptic lililowaua watu 45.

Francis amepangiwa kukutana na Sheikh Ahmed al-Tayeb, Imamu mkuu wa Serikali ya Misri-inayoendesha Msikiti wa al-Azhar siku ya Ijumaa, kabla ya kufanya mazungumzo baadaye na Rais Abdel Fattah el-Sisi na Kiongozi wa Kanisa la Coptic nchini Misri, Pope Tawadros.
Francis alipokewa uwanja wa ndege wa Cairo na waziri mkuu wa Misri, Sharif Ismail.

Papa amewaambia waandishi wa habari kuwa ziara yake ni safari ya udugu na umoja, na ziara hiyo itadumu kwa siku mbili, lakini amekiri kwamba itakuwa na “mambo mengi.”

Misri bado iko katika hali ya hatari baada ya shambulizi hilo la bomu kwenye kanisa la Coptic mapema mwezi huu, na usalama utazidi kuimarishwa katika makanisa kufuatia ziara ya Pope. Pia Francis ataongoza ibada siku ya Jumamosi.

XS
SM
MD
LG