Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:02

Korea Kusini yakataa kubebeshwa mzigo wa dola bilioni 1


Mfumo wa kujikinga na makombora (THAAD)
Mfumo wa kujikinga na makombora (THAAD)

Serikali ya Korea Kusini imekataa mara moja wito wa Rais Donald Trump ukiitaka Seoul kulipa dola bilioni moja kwa ajili ya mfumo wa kujihami na makombora (THAAD) unaowekwa na Marekani nchini humo.

Wizara ya Ulinzi imetoa tamko Ijumaa ikisema, “ Hakuna mabadiliko katika msimamo wa Korea Kusini na Marekani kuwa serikali yetu itatoa ardhi na nyenzo nyingine za kusaidia mfumo huo na Marekani itagharimia mfumo wa THAAD unaowekwa, uendeshaji na matengenezo yake.

Kuwekwa kwa mfumo wa kujihami (THAAD) wenye kuweza kutungua makombora ulikubaliwa mwaka jana na serikali ya aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama na aliyekuwa Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.

Hata hivyo Park aliweza kuepuka madai kwamba atatakiwa kuliomba Bunge la Taifa kupitisha mradi huu kwa kudai kuwa hakuna gharama za ziada zitazotakiwa kutolewa kwa ajili ya kuweka mfumo huo wa THAAD.

Aliyekuwa afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani amekadiria kuwa gharama za mfumo huo ni dola bilioni 1.2, na kusema kuwa Marekani hawatotaka kuiuzia Seoul mfumo huo wa THAAD.

Trump pia amesema akiwa ofisi ya Oval wakati wa mahojiano anataka kutatua tatizo hili kwa amani, ikiwezekana kupitia vikwazo vipya vya uchumi, na kuongeza kuwa, “ Kuna uwezekano tukaishia kuwa na mgogoro mkubwa, mkubwa na Korea Kaskazini.”

China imeiambia Washington kwamba imeikanya Pyongyang kuwepo vikwazo vipya vya uchumi kutoka China iwapo itajaribu kufanya jaribio jingine la nyuklia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson ameiambia Fox News katika mahojiano Alhamisi. Hilo litapelekea Beijing kubadilisha msimamo, ambayo imekuwa hadi sasa haikotayari kuweka vikwazo zaidi ya vile vilivyo amrishwa na Umoja wa Mataifa.

Msemaji mmoja wa wizara ya mambo ya nje wa China amekataa kuthibitisha au kukanusha kauli ya Tillerson Ijumaa, akitupilia mbali swali hilo wakati wa kutoa muhtasari kuwa ni “dhana” Shirika la habari laAssociated Press limerepoti.

XS
SM
MD
LG