Wakati Francis akiwa anatayarisha vipaumbele vyake viwili katika ziara yake kuanzia Jumapili hadi Jumanne akizuru Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuhimiza mazungumzo baina ya imani mbalimbali na kutembelea vituo vya Wakatoliki – kuna uwezekano protokali ya kidiplomasia ikamlazimisha kutogusia malalamiko kadhaa mengine.
UAE kuunga kwake mkono vita vilivyo anzishwa na Saudi Arabia huko nchini Yemen, ambavyo vimesababisha mgogoro wa kibinadamu mkubwa kuliko yote duniani, na pia rikodi tata ya haki za binadamu dhidi ya UAE na uvunjifu wa sheria za kazi kuna uwezekano mkubwa kutozungumziwa hadharani wakati wa ziara hiyo.
Kongamano kuzikutanisha dini mbalimbali
Papa Francis anaelekea Abudhabi kuhudhuria kongamano litakalowaleta waumini wa dini mbalimbali pamoja unaodhaminiwa na kikundi cha Baraza la Wazee wa Kiislam kilicho na makao yake UAE, ni juhudi zilizoanzishwa ili kukabiliana na misimamo mikali ya dini ikiwa ni juhudi ya kueneza Uislam kwa hekima na sio kwa kutumia mabavu.
Kongamano hilo ni wazo la Sheikh Ahmed el-Tayeb, kiongozi mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambacho kinaheshimika kwa mchango wake mkubwa wa miaka 1,000 katika kutoa mafunzo ya Kiislam ya madhehebu ya Sunni kwa maimamu na wanazuoni kutoka ulimwenguni kote.
Mahusiano yarejea kuwa mazuri
Huu utakuwa ni mkutano wa tano kati ya Francis na el-Tayeb, ikiwa ni ushahidi tosha kwamba kusitishwa kwa mahusiano kati ya Al-Azhar na Vatican kulikotokana na matamko ya Papa Benedict XVI 2006 kauli iliyokuwa inahusisha dini ya Uislam na uvunjifu wa amani ikiwa sasa uhusiano huo unarejea kuwa mzuri.
Katika ujumbe wa Video kwa uongozi wa UAE katika kilele cha ziara yake, Francis amempongeza “rafiki yake na ndugu yake” el-Tayeb na kusifia ushujaa wake wa kuitisha mkutano huu ili kutangazia dunia “Mungu anatuunganisha na wala hatugawanyi.”
Mkutano wa kihistoria
“Nimefurahishwa sana na mkutano huu ambao Mungu ametupa fursa ili tuandike, katika ardhi yenu tukufu, kurasa mpya ya historia ya mahusiano kati ya dini na kuwa ni uthibitisho kwamba sisi ni ndugu pamoja na kuwepo tofauti kati yetu,” Francis amesema.
Katika tamko lake Jumamosi, Al-Azhar imeeleza kuwa mkutano ujao ni wa “kihistoria” na kupongeza “uhusiano wa udugu wa kweli” kati ya imam na papa, ambapo umesema umeendelea hata katika kutumiana pongezi za siku zao za kuzaliwa.