Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:36

Papa Francis asisitiza amani Jerusalem


Papa Francis
Papa Francis

Papa Francis ametoa wito juu ya umuhimu wa “kuwepo amani Jerusalem” na “pande zote kuaminiana” katika Rasi ya Korea wakati akiangaza madhila yanayowakabili watoto katika maeneo yenye vita ulimwenguni.

Katika hotuba yake ya kusherehekea Krismas maarufu kama “Urbi et Orbi” (ikimaanisha kwa mji na dunia nzima), papa amehutubia kutoka katika varanda yake iliyoko katikati ya Kanisa la Mtakatifu Peter huko Rome.

Francis alizungumzia “kuongezeka kwa mivutano kati ya Waisraeli na Wapalestina”, akieleza matumaini yake kuwa “moyo wa kuanza mazungumzo pengine utakuwepo kati ya pande zote na mazungumzo ya kufikia suluhisho huenda hatimaye yakafikiwa, ambayo yatawezesha kuwepo maelewano ya kuwepo mataifa mawili yakiishi pamoja Mashariki ya Kati.

“Na tuombe kwa pamoja kwamba mvutano uweze kumalizika katika Rasi ya Korea na uwezekano wa kuongezeka kuwepo kuaminiana kati ya pande mbili kwa maslahi ya dunia kwa ujumla,” Papa amesema.

Wakati huohuo vyanzo vya habari Vatican vimeripoti kuwa Papa Francis amewahimiza waumini wa kanisa la Roma Katoliki kuwafariji mamilioni ya wahamiaji ambao wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na kutokuwepo amani katika nchi zao.

Alieeleza kuwa wahamiaji wengi wanalazimika kukimbia utawala wa kidikteta ambao unapuuzia suala la amani na kutojali umagaji damu usion na hatia.

Papa Francis ameweka msisitizo maalum katika uongozi wake suala la utetezi wa wahamiaji.

XS
SM
MD
LG