Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:34

Wakimbizi wa kambi ya Dadaab warejea Somalia…


Baadhi ya wakimbizi wakiondoka kuelekea Somalia
Baadhi ya wakimbizi wakiondoka kuelekea Somalia

Wakimbizi waliopewa hifadhi nchini Kenya katika kambi ya Dadaab, baada ya taifa la Somalia kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 27 iliyopita, sasa wameanza safari ya kurejea nchini Somalia.

Ingawaje wengi kati ya wakimbizi hao wanaonelea ni wakati muwafaka sasa kurudi Somalia, baadhi yao wanadai kuwa wamelazimika kurudi nyumbani kwa kukosa uhuru wa kutembea na maisha yao yanazidi kurudi nyuma kutokana na hali ngumu ya maisha kambini.

Zoezi la kuwarudisha wakimbizi ilianza mwaka 2016, ambapo wakimbizi hao walitakiwa kuondoka kwa hiari yao wakati watakapo jiridhisha kuwa hali ni shwari nchini Somalia.

Kwa mujibu wa shirika la UNHCR ambalo husimamia masuala ya wakimbizi ...shirika hilo huwapa fedha ya kuanza maisha upya tena [pindi watakapo fika Somalia] na kila baada ya miezi sita wao huwatembelea huko waliko.

Hata hivyo shirika hilo limesimamisha mpango wa kuwapeleka wakimbizi waliokuwa wakiishi sehemu za Baidoa kutokana na hali ya ukame na vilevile kwa sababu ya milipuko ya magonjwa mbalimbali.

Japokuwa wapo wakimbizi ambao hurejea tena kambini nchini Kenya kwa madai kuwa Somalia siyo salama, na hivyo shirika la UNHCR hufanya uchunguzi kubaini kuwa taarifa hizo ni za ukweli.

Kambi ya dadaab na hagadera ilikuwa na wakimbizi Zaidi ya elfu mia nne hata hivyo tangu mpango huo kuanza ni waimbizi elfu mia mbili waliosalia .

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Hubbah Abdi, Kenya

XS
SM
MD
LG