Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:02

Sitarudi kamwe Somalia- Mkimbizi


Watoto wa Mama Jamila katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
Watoto wa Mama Jamila katika kambi ya Dadaab nchini Kenya

Mwanamke mkimbizi ambaye amerudi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya alinusurika chupuchupu katika mlipuko mkubwa uliotokea nchini Somalia Octoba 2017.

Mama Jamila Hassan alirudi nchini Somalia kwa hiari yake lakini baada ya shambulizi hilo nchini Somalia hivi sasa amerudi tena kambini na taarifa za kusikitisha na kuapa kamwe hatarudi tena Somalia.

Mwandishi wa VOA anaripoti kuwa wakati wakiwa wameketi nje ya nyumba ya mama Jamila ambayo ni ya muda ...walilazimika kukatiza mahojiano ili kumruhusu atulie baada ya machozi kuanza kumbubujika akielezea jinsi shambulizi la Okotoba 2017 lilivyotokea mbele yake jambo ambalo hawezi kulisahau maishani mwake.

“Nilikuwa naishi mita chache na sehemu iliyoshambuliwa, niliona miili iliyokuwa imekatika katika ikiondolewa kwenye vifusi vya jengo lilokuwa limeripuliwa, picha ya kutisha ambayo bado inaendelea kunisonga akilini mwangu na sitamanikukumbuka niliokuwa nimeyashuhudia,” aliyasema haya huku akifuta machozi yake.

“Wakati bomu hilo lililipuka baadhi yay a watoto walikuwa wakicheza nje , fikra iliyonjia ya kwanza ni kuwa wao wamefariki kwenye shambulizi lakini nashukuru mungu waliepuka shambulizi hilo” akaongoza.

Katika mahojiano maalum yaliyofanywa na VOA, Mama Jamila amesema shambulizi la okotoba 14 lililowauwa zaidi ya watu 400 na kuufanya moyo wake unyong’onye na hivyo kutotaka kamwe kurudi katika nchi aliyozaliwa baada ya yeye na familia yake kuponea chupuchupu shambulizi hilo ni sawa na maajabu ya mtu kuweza kupita katika tundu la sindano.

Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya
Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya

Mama Jamila mwenye watoto nane ambaye sasa yuko katika kambi ya Dadaab amesema mume wake Ayub Hassan alipatwa na mshtuko wa moyo hadi kufikia leo hawezi kuzungumza na amebakia kitandani kutokana na athari ya mlipuko huo alioshuhudia mjini Mogadishu.

Aliiambia VOA kuwa , wakati tangazo la kuwataka wakimbizi kurejea nchini Somalia kwa hiari yao lilipotangazwa, yeye na familia yake walijiandikisha ili kusafiri kurejea nyumbani baada ya kuhakikishwa kuwa usalama umeimarishwa.

Kwa mujibu wa maelezo yake alisafiri kuelekea nchini Somalia Aprili 2016 na kutua mjini Mogadishu baada ya kukimbia mji huo kufuatia vita ya mwaka 2010 na kuishi hadi pale shambulizi lilipo fanyika na kuzibamatumaini yake ya kurejea tena Somalia.

Alirejea tena kambini mwezi Novemba 2017 huku akielezea alivyoteseka kurudi kupitia njia za mkato huku akikabiliwa na ubaguzi kutoka kwa wakimbizi wenzake ambao ulimnyongesha roho zaidi na kutonesha kidonda cha moyoni kilichotokana na shambulizi hilo.

“Sitarudi tena Somalia hata kama kambi hii itafungwa, nitabakia hapa pekee yangu ambapo siwezi kusikia sauti ya milipuko kila wakati na hata sitaki kukumbuka niliyoyapitia Somalia,” alielezea VOA katika kambi ya Dadaab.

Akiwa amembeba mwanawe mwenye umri wa miezi mitatu na huku akiwa amezungukwa na wanawe wengine, mama Jamila sasa anaishi akiwaomba wakimbizi wenzake chakula kwani tangu aliporejea kambini hajasajiliwa tena na shirika la kusimamia wakaimbizi la UNHCR.

“Nilipewa kadi na shirika la UNHCR lakini hadi kufikia sasa sijasikia lolote kutoka kwao na sasa natengemea majirani ambao kwa imani zao na ukarimu wao wameendelea kunisaidiachakula mimi na watoto wangu,“ amesema.

Afisa anayesimamia masuala ya wakimbizi Denis Alma Kuindje amesema wanataarifa kuwa wapo wakimbizi ambao waliondoka kambini kwa hiari yao na wamerudi tena kama wakimbizi. Dennis aliongeza kuwa wale wakimbizi ambao wamerejea tena hutafutwa ili kupokea taarifa zao na pia kujua sababu iliyopelekea wao kurudi tena katika kambi ya Dadaab.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Hubba Abdi, Kenya

XS
SM
MD
LG