Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa vijana hao Abdiweli Jama and Abdirahman Hussein waliletwa kambini miaka 11 iliyopita baada ya kutoroka vita iliyoisambarartisha nchi ya Somalia kwa miongo kadha.
Kwa upande wake Shaffe Abdullahi, ambaye ni mwenyekiti wa shule ya waberi, ambapo vijana hao walikuwa wanafunzi, anadai kuwa “ukosefu wa walimu , vifaa vya kusomea na hali ngumu ya maisha kambini zilikuwa ni changamoto za kutosha kwa wahitimu hao…. Hata hivyo matokeo mazuri ya vijana hao yametufurahisha.
Ameongeza kuwa: “Wanafunzi wengi hufanya vizuri katika masomo yao lakini hubakia kambini kwa kukosa msaada wa kujiunga na vyuo vikuu na hulazimika kufanya kazi ya ualimu katika shule za wakimbizi japokuwa hawajapata mafunzo yoyote ya ualimu… hivyo basi tunatoa wito kuwa tunaomba msaada ili wanafunzi hawa waliofanya vizuri watimize ndoto yao.”
Imetayarishwa na mwandishi wetu Hubbah Abdi, Kenya