Papa Francis anajaribu kutafuta suluhisho kwa mzozo wa kisiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwaita viongozi wa kanisa walokua wanaongoza juhudi za upatanishi kati ya serikali ya Joseph Kabila na upinzani, juu ya hatua za kuchukuliwa baada ya muda wa Kabila wa Jumatatu tarehe 19 unafika.
Mkuu wa Kanisa la Katholiki alichukua hatua hiyo baada ya viongozi wa kidini kukutana na Rais Kabila siku ya Ijuma na kiongozi wa upinzani Étienne Tshisekedi, bila ya kupata ufumbuzi.
Muungano wa upinzani wa "Ressmblemement" unampango wa kuitisha maandamano Jumatatu ambayo Wakongo wengi na Jumia ya kimataifa wanahofu yanaweza kuzusha ghasia nchini humo.
Inaripotiwa kwamba mazungumzo kati ya pande mbili yanatazamiwa kuanza tena siku ya Jumatano.
Kwa upande mwengine afisa wa juu wa Ressemblement anamhimiza Rais Joseph kabila kufikia makubaliano na kundi hilo na kuacha madaraka ili kuruhusu kipindi cha amani cha kukabiliana madaraka.
Muda rasmi wa mhula wa Kabila unamalizika jumatatu tarehe 19.
Freddy Mbuyamu Matungulu kiongozi wa kundi la Nabiso Kongo, "Kongo Yetu", anasema viongozi wa mungano wa Ressemblement wanakutana Kinshasa kuamua utaratibu wa mpito na hali ya baada ya muda wa Kabila kupita.