Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anatarajiwa kutembelea pia Bangladesh Alhamisi
Ziara ya papa haihusishi ratiba yake katika kambi za wakimbizi, lakini anatarajiwa kukutana na kikundi kidogo cha watu wa Rohingya huko Dhaka, makao makuu ya Bangladesh.
“Ninakuja kutangaza neno la Yesu Kristo, ujumbe wa upatanishi, kusameheyana na amani,” Pope Francis ameiambia radio Vatican, “Ziara yangu inakusudia kuthibitisha kuwa jumuiya ya Wakatoliki Myanmar inashikamana na kumuabudu Mungu na kushuhudia neno la Mungu.”
Katika wiki za karibuni, Myanmar na Bangladesh walikubaliana kuwarudisha mamia ya maelfu ya Warohingya waliokimbia Bangladesh kuepuka vita katika jimbo la Rakhine huko Myanmar, kwa mujibu wa maafisa wa nchi zote mbili.
Pamoja na makubaliano hayo, Kardinali Patrick D'Rozario ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa hali imeendelea kuwa "ngumu na tata katika kupata ufumbuzi."
"Natumai kuwa Warohingya wataweza kurudi Myanmar," Askofu Mkuu D'Rozario wa Dhaka, ameiambia shirika la habari la AFP.