Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:30

Papa Francis ataka tafsiri ya Sala ya Bwana kubadilishwa


Papa Francis
Papa Francis

Papa Francis amesema fafsiri ya hivi sasa yenye maneno yanayosema “ Usituongoze katika majaribio” si tafsiri nzuri, kwa sababu Mungu hawaongozi wanadamu katika kutenda dhamb.

Amependekeza kutumika “ utukinge tusiangukie katika majaribio” badala yake, Papa ameiambia Televisheni ya Italy Jumatano usiku. Sala ya Bwana ni sala maarufu sana katika Ukristo.

Papa amesema Kanisa Katoliki Ufaransa hivi sasa linatumia tafsiri mpya “Utukinge tusiangukie katika majaribio” badala yake, na tafsiri inayofanana na hii itumike ulimwenguni kote.

“Unikinge mimi nisiangukie katika majaribio kwa sababu ni mimi ambaye ninateleza, na siyo Mungu ambaye ananitupa mimi katika majaribio na kisha kuniangalia ninavyo anguka,” ameiambia TV 2000, idhaa ya televisheni ya Kikatoliki Italia. “Baba hafanyi hivyo, Baba anakusaidia kunyanyuka mara moja.

Tangu alipochaguliwa kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis hajachelea kukabiliana na malumbano na ameweza kutatua baadhi ya mambo mapema kabisa, wachambuzi wa Vatican wameeleza.

XS
SM
MD
LG