Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:52

Papa asisitiza mapadri waharibifu wasivumiliwe Ireland


Papa Francis akizungumza mjini Dublin katika ziara yake ya kwanza Ireland. Agosti 25, 2018.
Papa Francis akizungumza mjini Dublin katika ziara yake ya kwanza Ireland. Agosti 25, 2018.

Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis ameanza ziara ya kwanza ya cheo alichonacho kwenda Ireland baada ya takribani miaka 40 na kuelezea kile alichozungumza na jamii ya wakatoliki kufuatia uhalifu usiokubalika uliofanywa na baadhi ya mapadri.

Papa Francis ameuambia mkusanyiko huo "nashindwa kuelezea kadhia ya aibu iliyofanywa Ireland ya kuwanyanyasa vijana, ambayo ilifanywa na waumini wa kikatoliki wenye jukumu la kuwalinda na kuwapa elimu."

Papa Francis aliuambia mkusanyiko kwenye mapokezi ya kitaifa huko Dublin Castle, mahala ambako baadhi ya waathirika wa unyanyasaji huo walikuwepo “nashindwa kuelezea kadhia ya aibu iliyofanywa Ireland ya kuwanyanyasa vijana iliyofanywa na waumini wa kikatoliki wenye jukumu la kuwalinda na kuwapa elimu".

Katika juhudi za kuelezea dunia machungu kuhusu kadhia ya ngono, Francis alielezea hatua zilizochukuliwa na mtangulizi wake Papa Benedict kukabiliana na tatizo hilo.

Aliendelea kusema kwamba Papa Benedict hakukubali makosa yaliyotokea Vatican na muendelezo wa jaribio la kuzuia watu wanaoelezea ukweli.

Hata hivyo Papa Francis hakutoa mpango wa hatua zozote mpya zitakazo chukuliwa kuwaadhibu mapadri ambao wanashindwa kulinda parokia zao.

Ziara hii imekuja siku kadhaa baada ya Papa kutuma barua kwa Wakatoliki duniani akijibu matukio yaliyo dhihirika hivi karibuni ya unyanyasaji wa kigono yaliofanywa na mapadri.

Hivi karibuni ripoti ya washauri wa mahakama ya Marekani wamesema zaidi ya mapadri 300 waliohusika na unyanyasaji wa kingono waliwaharibu watoto 1000 katika dayosisi sita za Pennsylvania kwa kipindi cha miaka 70.

“Hata hivyo inafahamika kuwa vitendo hivi vya unyanyasaji vilifanyika siku za nyuma, lakini kadri muda ulivyopita tumekuja kujua maumivu ya wengi walioathiriwa na vitendo hivi,” Francis alisema katika barua yake.

Amesema kuwa kwa “fedheha na kutubia” Kanisa Katoliki linakiri halikuchukuwa hatua wakati muwafaka na inatambua kiwango cha hasara ambayo vitendo hivyo vya unyanyasaji vimewasababishia watu wengi.

Francis amesema “ hakuna juhudi yoyote ya kuomba msamaha na kuondoa madhara yaliyofanyika kamwe zinazoweza kujitosheleza.”

XS
SM
MD
LG