Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:00

Papa Francis ataka walio dhulumiwa kusikilizwa


Papa Francis
Papa Francis

Uongozi wa Vatican umesema kwamba tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizo ripotiwa dhidi ya wachungaji wa dhehebu la Katoliki Jimbo la Philadelphia, Marekani ni makosa ya uhalifu na uovu mkubwa wa maadili.

Taarifa ya Vatican ilitolewa katika ripoti ya wapelelezi, Alhamisi, inasema kwamba kiongozi wa Kanisa la Katoliki duniani papa Francis yuko upande wa zaidi ya watu 1000 wanaodai kudhulumiwa katika kipindi cha miongo kadhaa katika jimbo hilo.

Kulingana na taarifa ya Vatican, Papa Francis amehimiza Kanisa Katoliki kuwasikiliza wote waliodhulumiwa ili kusaidia kukabiliana na uovu huo alioutaja kuwa wa kutisha na ambao umeharibu maisha ya watu wengi wasio na hatia.

XS
SM
MD
LG