Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:49

Papa Francis ataka Kanisa Katoliki kutowavumilia mapadri waharibifu


Papa Francis
Papa Francis

Papa Francis amesema Jumatatu kila juhudi lazima ifanyike kuhakikisha utamaduni wa Kanisa Katoliki unazuia siku za usoni vitendo vya unyanyasaji wa kingono vinavyo fanywa na mapadri kwa watoto na iwapo unyanyasaji huo utafanyika iwepo mikakati ya kuweka wazi udhalilishaji huo.

Maelezo ya papa yamekuja katika barua aliyoituma kwa Wakatoliki duniani akijibu matukio yaliyo dhihirika hivi karibuni ya unyanyasaji wa kigono yaliofanywa na mapadri.

Wiki iliyopita, ripoti ya washauri wa mahakama ya Marekani wamesema zaidi ya mapadri 300 waliohusika na unyanyasaji wa kingono waliwaharibu watoto 1000 katika dayosisi sita za Pennsylvania kwa kipindi cha miaka 70.

“Hata hivyo inafahamika kuwa vitendo hivi vya unyanyasaji vilifanyika siku za nyuma, lakini kadri muda ulivyopita tumekuja kujua maumivu ya wengi walioathiriwa na vitendo hivi,” Francis alisema katika barua yake.

Amesema kuwa kwa “fedheha na kutubia” Kanisa Katoliki linakiri halikuchukuwa hatua wakati muwafaka na inatambua kiwango cha hasara ambayo vitendo hivyo vya unyanyasaji vimewasababishia watu wengi.

Francis amesema “ hakuna juhudi yoyote ya kuomba msamaha na kuondoa madhara yaliyofanyika kamwe zinazoweza kujitosheleza.”

XS
SM
MD
LG