Papa amesema wakati akiwa katika sehemu takatifu huko Knock, Ireland, Jumapili kuwa kashfa hiyo “kidonda kilicho wazi” na “hatua thabiti na imara” lazima zichukuliwe kutafuta “ukweli na haki.”
Francis pia amelikaripia kanisa nchini Ireland jinsi kwa miongo mingi iliyopita taasisi za nchi hiyo zilizokuwa zinaendeshwa na Wakatoliki walivyo wachukuwa watoto waliopatikana nje ya ndoa na kuwalea. Kitendo hicho kiliwanyang’anya watoto hao maadili yao, wakiwaacha watoto hao “kutelekezwa” na “kuwa na kumbukumbu zenye kuwahuzunisha.”
Wito wa Francis wa kuleta toba umekuja wakati Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano alipoandika barua iliyochapishwa katika gazeti la wakatoliki la Taifa, National Catholic Register.
Katika barua yake yenye kurasa 11, Vigano, balozi wa Vatican mstaafu aliyekuwa Marekani, anamshutumu Francis na maafisa wengine wa Vatican kwa kupuuzia madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Kadinali wa Marekani Theodore McCarrick ambaye alilazimishwa kustaafu mwezi Julai baada ya uchunguzi uliofanywa na kanisa kugundua madai ya watoto wadogo walionyanyaswa kingono kuwa ni ya kweli.
Vigano alimwambia Francis mwaka 2013 madai kuhusu McCarrick kuwaharibu wanafunzi waliokuwa wanasomea upadri, lakini Francis aliondoa adhabu aliyopewa McCarrick ambayo ilitolewa na Papa Benedict.
"Yeye [Papa Francis] alikuwa anajua angalau kuanzia Juni 23, 2013 kuwa McCarrick alikuwa ni mharibifu mzoefu wa watoto," Vigano ameandika, akiongeza kuwa " alikuwa anajuwa kuwa McCarrick alikuwa ni mtu fisadi, na kumlinda mpaka mwisho huu wenye machungu."
Francis atamaliza ziara yake Ireland Jumapili kwa kuendesha ibada ya umma huko Dublin katika uwanja wa Phoenix.