Ofisi ya masuala ya kibinadamu ya UN imesema Alhamisi nchi maskini duniani hazitegemewi kufikia kilele cha maambukizi ya COVID-19 mpaka baada ya miezi mitatu au sita, lakini tayari nchi hizo zinashuhudia ukosefu wa ajira na kipato, pamoja na mgawanyo finyu wa mahitaji ya chakula na watoto wakiwa hawapati chanjo za kawaida.
Ombi la awali lilikuwa kupata ufadhili wa dola bilioni 2, na shirika hilo limesema Alhamisi linahitaji jumla ya dola bilioni 6.7.
“Iwapo hatutawasaidia watu maskini sana – hasa wanawake na wasichana na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatari – wakati wakikabiliana na janga hili na athari za kudorora kwa uchumi wa dunia, sote tutakuja kukabiliana na athari zinazotokana na janga hili kwa miaka mingi inayokuja. Na hilo litakuwa na machungu zaidi, na gharama yaka itakuwa kubwa, kwa kila mtu,” amesema Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu wa UN, Mark Lowcock.
Ombi hilo la msaada linaloendelea linajumuisha nchi tisa kwenye orodha ya mataifa yaliyo katika hatari zaidi : Benin, Djibouti, Liberia, Msumbiji, Pakistan, Ufilipino, Sierra Leone, Togo na Zimbabwe.
Nchi kadhaa tayari zimeanza kulegeza masharti ya kutotoka nje yaliyokuwa yamewekwa kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kwa kipindi cha miezi michache iliyopita, wakati maafisa wakiwa na matumaini kuwa hali mbaya kuliko zote ya maambukizi imepita katika mataifa yao.
Lakini wataalam wa afya wanaonya kuwa kuna uwezekano wa maambukizi hayo kuibuka tena iwapo amri hizo za kutotoka nje zitaondolewa kwa haraka.
“Tunajiaminisha kuona maambukizi yakirejea tena ambayo hatutaweza kuyahimili,” amesema Dkt Ian Lipkin wa Chuo Kikuu cha Columbia, New York.
Serikali za Ulaya na baadhi ya majimbo ya Marekani ni miongoni mwa sehemu ambazo zimeruhusu aina fulani ya biashara kufunguliwa tena, na kuruhusu watu kwenda kwenye migahawa na madukani lakini kwa sharti la kuepuka misongamano na kutokaribiana na watu wengine.
Maafisa wa afya wameeleza masikitiko yao kuwa umma utaangalia hatua hiyo kama ni dalili ya kuwa tishio la virusi haliko tena.
South Korea is taking new steps as its number of new infections remains around zero. Its largest airline said Thursday it would resume flights to the United States, Europe and other parts of Asia next month.
Korea Kusini inachukuwa hatua mpya wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuwa sifuri. Shirika la kubwa la ndege limesema Alhamisi litaanza safari zake kwenda Marekani, Ulaya na nchi nyingine za Asia mwezi ujao.
The South Korean government is also expanding shipments of masks to other countries, with a focus on those with an urgent need amid larger outbreaks of COVID-19.
Serikali ya Korea Kusini inaendelea kuongeza idadi ya barakoa inazopeleka nchi nyingine, ikilenga zile ambazo zinahitaji kwa haraka kutokana na milipuko mikubwa zaidi ya maambukizi ya COVID-19.
In Brazil, the health ministry reported a record rise of 10,500 new confirmed cases, pushing the country’s total above 125,000.
Nchini Brazil, wizara ya afya imeripoti kuongezeka kwa maambukizi mapya 10,500 yaliyothibitishwa, na hivyo idadi ya maambukizi kufikia 125,000.
There are about 3.8 million confirmed cases worldwide, with 264,000 deaths.
Tayari kuna watu milioni 3.8 waliopimwa na kuthibitishwa kuwa na maambukizi duniani kote, wakati idadi ya vifo ikifikia 264,000.
Mwisho