Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:08

WHO : Idadi ya maambukizi Afrika yaweza kuongezeka kungekuwapo vifaa vya kutosha kupima COVID-19


Mfanyakazi akiwa katika mavazi ya kujikinga na virusi vya corona akiweka dawa ya kuzuia virusi vya corona kusambaa katika bustani katikati ya mji baada ya mlipuko wa COVID-19 jijini Algiers, Algeria Machi 23, 2020.
Mfanyakazi akiwa katika mavazi ya kujikinga na virusi vya corona akiweka dawa ya kuzuia virusi vya corona kusambaa katika bustani katikati ya mji baada ya mlipuko wa COVID-19 jijini Algiers, Algeria Machi 23, 2020.

Shirika la Afya Duniani limeripoti Ijumaa kuwa maambukizi ya COVID-19 barani Afrika yameongezeka kwa asilimia 51 na vifo vimefikia asilimia 60.

Akiongea katika mkutano wa Geneva, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, amesema idadi hiyo inaweza kuwa ya juu zaidi kama upimaji ungekuwa wa kutosheleza barani Afrika.

“Wiki iliyopita kumekuwa na ongezeko la asilimia 51 katika taarifa za idadi ya maambukizi zilizo ripotiwa katika bara langu, Afrika, na asilimia 60 ya ongezeko la vifo. Kutokana na changamoto za hivi sasa za kupata vifaa vya kupima COVID-19, inawezekana kuwa idadi halisi iko juu kuliko kile

Hadi kufikia siku ya Ijumaa, takwimu rasmi zinaonyesha, Algeria, ambayo inavifo zaidi ya 360 hadi sasa, ni nchi ya Kiafrika iliyokuwa na idadi ya juu zaidi ya vifo. Misri ni ya pili ikiwa na zaidi ya vifo 200. Morocco imeripoti vifo 135 na Afrika Kusini 50.

Nchi za Kiafrika zimethibitisha kuwa na jumla ya maambukizi 19,334 tangu mlipuko wa virusi hivyo kutokea China mwisho wa mwezi Disemba 2019.

Japokuwa hadi sasa Afrika imekuwa na maambukizi machache ukilinganisha na maeneo mengine ya dunia, maafisa wa afya wanahofia kuwa hali hiyo inaweza kugeuka na kuwa mbaya zaidi.

XS
SM
MD
LG