Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:54

Idadi ya vifo kutokana na Corona yapungua Italia


Mgonjwa akipimwa virusi vya Corona
Mgonjwa akipimwa virusi vya Corona

Italy imerekodi kiwango cha chini zaidi cha vifo kutokana na maambukizi ya Corona, katika kipindi cha wiki tatu.

Maafisa nchini Italy, wamesema watu 431 wamekufa kutokana na Corona na hivyo kujumulisha idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa huo kufikia elfu 19,899.

Idadi ya watu 431, ndio ya chini zaidi tangu March 19. Idadi ya watu wanaolazwa katika vyumba vya wagonjwa mahtuti imepungua kwa siku ya tisa mfululizo.

Idadi ya watu wanaolazwa hospitalini nayo imepungua kwa kiasi kikubwa, hali inayoleta matumaini ya kukabiliana na virusi vya Corona nchini humo.

Nchi hiyo inaingia wiki ya nne ya kusitisha shughuli zake zote na watu kusalia nyumbani, ili kuzuia maambukizi.

Maafisa wameripoti kwamba shughuli ya kuwapima watu imeongezeka nchini humo, na wanaopatikana kuambukizwa kutakiwa kukaa nyumbani kabisa na kujitenga na watu wengine.

Zaidi ya watu milioni moja wamefanyiwa vipimo vya Corona nchini Italy.

Watu 156,363 wamethibitishwa kuambukizwa, japo maafisa wanasema kwamba huenda idadi ya watu walioambukizwa ni mara 10 zaidi ya idadi inayojulikana, hasa katika mji ambao umeathirika zaidi wa Lombardy.

Maafisa wameonya kwamba huenda idadi ya vifo kutokana na Corona ni ya juu zaidi kuliko inavyojulikana, kwa kuzingatia vifo vilivyotokea katika sehemu maalum za kuwahudumia watu wazee, ambao hawakufanyiwa vipimo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG