Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:40

China yasema Marekani kusitisha ufadhili wake WHO kutaziathiri nchi zote


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

China imesema Jumatano kuwa uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha ufadhili kwa Shirika la Afya Duniani kutaziathiri nchi zote wakati dunia ikikabiliwa na hatua muhimu ya kupambana na janga la virusi vya corona.

Tamko la wizara ya mambo ya nje la nchi hiyo limekuja baada ya Trump kutangaza hilo Jumanne ambapo alisema kuwa WHO haikufanya uchunguzi wa kutosha juu ya ripoti za awali juu ya kuwepo mlipuko wa virusi hivyo nchini China.

Ujerumani

Ujerumani imejiunga katika kulitetea shirika hilo, huku Waziri wa Mambo ya Nje Heiko Maas akisema Jumatano kuwa kutoa lawama “hakutasaidia.”

“Inabidi tushirikiane kwa karibu katika kupambana na #COVID19, Maas alituma ujumbe wa Twitter. “Moja ya vitega uchumi bora ni kuiimarisha @UN, hususan @WHO ambayo haina ufadhili wa kutosha, kwa mfano kwa ajili ya kutengeneza na kusambaza vifaa vya kupimia na chanjo.”

Chuo Kikuu cha Johns Hopkins

Kuna takriban maambukizi milioni 2 yaliyothibitishwa duniani, lakini kutokana na tatizo la kuwepo vipimo katika maeneo mengi, kiwango cha maambukizi kwa kweli kiko juu zaidi. Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Jumatano kimeeleza idadi ya vifo ni zaidi ya 126,000.

Ufaransa, Itali na Uhispania

Ufaransa imesema idadi ya vifo ni zaidi ya 15,000, na kuifanya iwe ni nchi ya nne, ikiwemo Marekani, Itali na Uhispania.

Italina Uhispania ni kati ya nchi kadhaa za Ulaya ambazo zimeanza kulegeza masharti ya kutotoka majumbani yaliyokuwa yamewekwa kuzuia kuenea kwa virusi hivyo, wakati Ufaransa imeongeza mapema leo muda wa amri hiyo ya kutotoka majumbani.

Majadiliano juu ya lini na namna gani ya kulegeza masharti yanaendelea katika serikali mbalimbali duniani kote.

California

Katika jimbo la California lilioko magharibi mwa Marekani, Gavana wake Gavin Newsom amesema ataruhusu watu kutoka majumbani pale tu idadi ya watu wanaolazwa hospitalini kutokana na virusi vya corona itapopungua kwa angalau wiki mbili mfululizo, kuwepo kwa vifaa vya kutosha vya kujikinga kwa wafanyakazi wa afya, maafisa watakapokuwa na uwezo bora wa kufuatilia walioambukizwa na kuwatenganisha na jamii.

India

India imetangaza Jumatano mpango wake wa kuruhusu shughuli za uzalishaji viwandani na mashambani kuanza tena katika maeneo ya vijijini ifikapo Aprili 20, wakati amri ya kutotoka majumbani nchi nzima ikiendelea kutekelezwa mpaka mapema mwezi Mei.

Kutofautiana katika kuchukuliwa amri hizi zinaonyesha muelekeo wa mlipuko huu, wakati maeneo yaliyopata maambukizi mwanzoni yakionyesha dalili za kuridhisha kuwa janga hilo pengine litamalizika, wakati nchi nyingine zikianza kushuhudia kuongezeka kwa idadi ya maambukizi.

Afrika

Hilo limeonyeshwa na amri kadhaa mpya zilizotolewa wiki hii katika bara la Afrika. Malawi ni kati ya nchi zilizofanya hivyo hivi karibuni, wakati Rais Peter Mutharika alipotangaza Jumanne amri ya kutotoka majumbani kwa siku 21 kuanzia Jumamosi ijayo.

“Napenda kuwashauri kuheshimu kikamilifu amri hii kwa sababu ni kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu,” Mutharika amesema.

Kwa upande wa uchumi, amri ya kutotoka majumbani imepelekea kushuka zaidi kwa matumizi ya mafuta.

IEA

Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) limetoa makadirio yake Jumatano yakionyesha kushuka kwa mahitaji ya mafuta katika mwezi wa Aprili kwa mapipa milioni 29 kwa siku, kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha miaka 25.

New Zealand

Huko New Zealand, Waziri Mkuu Jacinda Ardern ametangaza kuwa yeye pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wamejitolea kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 katika hatua ya kukiri kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi ili kukabiliana na mlipuko wa corona.

XS
SM
MD
LG