Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:40

Maambukizi ya Corona yaongezeka Afrika


Kituo cha kutibu Corona
Kituo cha kutibu Corona

Wizara ya afya ya Tanzania imeripoti Jumatatu kuwa, watu takriban 14 zaidi wamepata maambukizi ya Covid-19.

Walioambukizwa wote ni raia wa Tanzania, 13 wakiwa Dar-es-salaam na mmoja mjini Arusha.

Wizara ya afya imeripoti kwamba juhudi za kufuatilia watu waliokuwa karibu na wagonjwa zinaendelea.

Wakati wa maadimisho ya pasaka, wakristo walikusanyika kanisani kwa maombi bila kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya.

Kuna mijadala kwenye mitandao ya kijamii Tanzania, kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibithi maambukizi nchini humo.

Nchini Afrika kusini watu 145 zaidi, wameambukizwa virusi vya Corona, na kujumulisha idadi ya watu 2,173 ambao wameambukizwa virusi vya Corona nchini humo.

Taarifa ya wizara ya afya hata hivyo haijasema idadi ya watu ambao wamekufa wala kupona kutokana na virusi vya Corona nchini humo.

Nchini Sudan, maafisa wameongeza mikakati zaidi ya kuzuia virusi vya Corona kusambaa.

Wamepiga marufuku usafiri wa magari kati ya miji na kutekeleza sheria za hali ya dharura ili kuhakikisha kwamba amri hizo zinatekelezwa.

Jumla ya watu 19 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Sudan kusini.

Nchini Liberia Vurugu zimeshuhudiwa wakati wa kutekeleza amri ya watu kutotoka majumbani, polisi wakitumia nguvu kuwalazimisha watu waliokuwa wanafanya shughuli za kujitafutia vitu muhimu za matumizi, kukaa makwao.

Hali ya kuchanganyikiwa ilionekana katika mji wa Monrovia, wenye jumla ya watu milioni 1, wengi wakisema kwamba walikuwa wamepata Habari kupitia mitandao ya kijamii kwamba serikali ilikuwa imetangaza watu kusalia majumbani mwao kuanzia saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili asubuhi, na wala sio kufunga shughuli zote kabisa.

Raia wa Liberia wana wasiwasi kwamba hatua hiyo ya rais George Weah, itaathiri zaidi Maisha ya watu katika nchi ambayo zaidi ya nusu ya watu ni maskini.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG