Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

Mjadala wa Chloroquine kuwa tiba ya COVID-19 washika kasi


Vidonge vya Chloroquine
Vidonge vya Chloroquine

Mjadala unaenelea nchi mbali mbali duniani juu ya dawa zinazotumiwa kwa muda mrefu kutibu malaria, Chloroquine zinaweza kuleta nafuu kwa wagonjwa wa COVID-19.

Mjadala umepata nguvu baada ya baadhi ya madaktari wa China na Korea Kusini ambako ugonjwa ulianzia kusema wagonjwa waliopewa dawa hiyo kwa mchanganyiko na dawa za antibiotics wameweza kupona haraka.

Hata hivyo waatalamu wengi wanatahadharisha wakisema uchunguzi zaidi wa kisayansi unahitajika kuhakikisha dawa hiyo inaleta mabadiliko.

Ufaransa baada ya daktari mashuhuri wa magonjwa ya kuambukiza Didier Raoult kutoka taasisi ya IHU mjini Marseille kujiondoa kutoka tume ya taifa ya kupambana na COVID 19 baada ya kusema mwishoni mwa mwezi wa Machi majaribio ya chloroquine kwa wagonjwa 36 wa COVID imepunguza sana idadi ya virusi mwilini mwa wagonjwa baada ya siku sita tu hapakuwa na virusi hivyo mwilini.

Baada ya malumbano alitoa majaribio ya watu 100 na matokeo sawa. Akisisitiza kwamba walitumia pia dawa ya arithromycin dawa ya kawaida kupambana na mambukizi ya bactiria.

Waatalaam wanabisha uchunguzi wa watu 34 hautoshi kusema ni utafiti wa kisayansi uliokamilika. Lakini Raoult anaamini ubishi unatokana na dhana ya makampuni ya dawa kuwa na tamaa ya kupata fedha nyingi.

Didier Raoult, Mkurugenzi ya taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ya Mediterranian, Ufaransa anasema : "Kuna hii hali ya shauku, ya lazima tupate dawa mpya. Lazima tupate chanjo mpya. Ukiwambia sikilizeni kuna hii dawa tunayo ifahamu na inafanya kazi vizuri ya Cloroquine, na isiyo ghali, wanakataa. Ninadhani ni suala la fedha tu."

Kutokana na shinikizo la waatalamu hivi sasa Ufaransa imeruhusu madaktari kutumia dawa hiyo kwa tahadhari katika hospitali peke yake.

Korea Kusini inatumia dawa hiyo kwa wagonjwa ambao wako taabani kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona na huko Profesa wa magonjwa ya kuambukiza Kim Woo Joo anathaadharisha pia utumiaji wake.

Kim Woo-joo, Profesa wa magonjwa ya kuambukiza anatema : "Ingawa chloroquine imekuwa ikitumiwa na wagonjwa wengi wa COVID 19 lakini athari na faida zake za kitatibu hazijathibitishwa kupitia utafiti. Utafiti wa kisayansi umeanza kuonyesha dalili kwamba choloroquine kwa hakika inatibu COVID-19.

Hapa Marekani kadhalika kumekuwa na mjadala mkali kati ya watalamu wa afya na Rais Donald Trump juu ya utumiaji wa dawa hiyo. Kongozi huyo alitangaza wiki mbili zilizopita kwamba dawa hizo zitaanza kutolewa New York na mwishoni mwa wiki alirudia kusema watu wanaweza kupewa dawa hiyo ambayo ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingawa haikufanyiwa majaribio.

Rais Donald Trump anasema : "Ninadhani watu wanabidi kupewa ikiwa uamuzi ni wangu. Huwenda nikafanya hivyo. Huwenda nikaitumia mimi mwenyewe. itabidi niwaulize madaktari kuhusu jambo hilo, lakini huwenda nikaitumia."

Huko Africa ambako dawa hiyo imekuwa ikitumika kwa miaka mingi kupambana na malaria watu wanakimbilia katika maduka ya dawa kununua kwa wingi hasa huko Afrika Magharibi. Nchini Burkina Faso Rasmane Ouedraogo amenunua za kutosha.

Rasmane Ouedraogo, mkazi wa Ouagadougou anaeleza : "Hata itakapo rasmishwa tuseme ikaidhinishwa kama dawa sahihi, basi nitakuwa tayari ninayo.

Mkuu wa idara ya magonjwa ya kuambukizwa katika hospitali ya Fann mjini Dakar Senegal Moussa Seydi anasema wametumia mchanganyiko wa dawa nyingine na zimeonesha dalili nzuri lakini anaonya.

Dkt. Mossa Seydi, Mku wa idara ya magonjwa ya kuambukiza Hospitali ya Fann, Dakar: "Wagonjwa wanaopewa matibabu maalum kwa kutumia Hydroxychloroquine wanapona kwa haraka sana. Lakini lazima ni sisitize kwamba utafiti wa kina wa kisayansi unahitajika kabla ya kuthibitisha dhana yeyote ile."

Burkina Faso Cameroon na Afrika Kusini zimeruhusu hospitali peke yake kutumia dawa hiyo. Lakini shirika la afya duniani linasema majaribio zaidi yanahitajika kwanza.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG