Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:16

WHO yahitaji dola milioni 130 kutoa huduma za dharura Zimbabwe


Mfanyakazi wa hospitali mjini Harare, Zimbabwe akichukua kipimo cha joto la dereva kabla ya kuingia ndani ya eneo la hospitali Machi 26, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo
Mfanyakazi wa hospitali mjini Harare, Zimbabwe akichukua kipimo cha joto la dereva kabla ya kuingia ndani ya eneo la hospitali Machi 26, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo

Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema linahitaji dola za Marekani milioni 130 kwa shughuli za huduma za dharura nchini Zimbabwe.

Hii inatokana na hali ya ukame na kudumaa kwa uchumi inayo sababisha upungufu mkubwa wa chakula nchini humo na hali kuwa mbaya zaidi kutokana na janga la virusi vya corona.

Mkurugenzi wa ofisi ya WHO Zimbabwe Eddie Rowe anasema wanahitaji fedha hizo kwa shughuli zao za dharura hadi mwezi wa Agosti ili kuepusha janga kubwa zaidi nchini humo.

Hadi sasa watu 11 tu ndio walioripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 lakini wataalamu wa uchumi wanatabiri inaweza kukabiliwa na kudumaa kwa uchumi kwa mara ya pili mfululizo 2020, pale janga hilo la afya litakapo sababisha shughuli zote za kiuchumi kusita.

Idadi ya maambukizi na vifo kutokana na janga la COVID 19 katika nchi zilizoathirika zaidi inaongezeka ambapo kulingana na takwimu za WHO kuna watu milioni moja laki tatu elfu 56 waloambukizwa kufikia Alhamisi.

Pia baadhi ya mashirika ya habari yameripoti kuwa idadi ya zaidi ya watu milioni 1.5 wameambukizwa.

Marekani inaendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wanaofariki kwa siku. Kwa siku ya mbili mfululizo jumla ya watu elfu mbili wamefariki na kufikisha idadi ya vifo toka mlipuko uanze nchini Marekani kufikia 14,831 kulingana na takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins hapa Marekani.

Hispania imeripoti kwa pande wake ongezeko kubwa la maambukizi kwa siku moja kufikia watu elfu 6,180 na kulingana na wizara ya afya ya nchi hiyo idadi ya maambukizi imefikia 150,000.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG