Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:05

Trump: Uamuzi wa kuruhusu shughuli kuanza Marekani ni 'Uamuzi Mgumu'


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump anasema uamuzi wa kuruhusu shughuli kuendelea nchini kama kawaida, “ ndio uamuzi mkubwa ambao sijawahi kukabiliwa nao.”

Amesema Ijumaa atajaribu kupima manufaa na madhara ya uamuzi huo akishirikiana na washauri wake wa afya na uchumi.

Hata hivyo, kile ambacho hakiko bayana hivi sasa ni iwapo majimbo yote yatafuata kile Trump atachosema. Trump hakusimamisha rasmi shughuli zote nchini, na alimwaachia kila gavana kufanya maamuzi katika jimbo lake. ,

Trump anasema anapendelea kuona shughuli zote zinaanza kama kawaida ifikapo Mei 1.

Dkt Anthony Fauci, mtaalam wa ngazi ya juu wa maradhi ya maambukizi, amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kuwa “hali ya maambukizi ya virusi vya corona ndio inayoweza kufanya maamuzi iwapo ni sahihi kuruhusu shughuli kufunguliwa au lau. Ametahadharisha kuwa maamuzi ya haraka yanaweza kupelekea wimbi jipya la maambukizi.

Wakati nchi nyingi duniani wananchi wanaendelea kutotoka majumbani ili kupunguza maambukizi ya janga la virusi, idadi ya maambukizi yanaendelea kuongezeka.

Kituo cha Johns Hopkins chenye kukusanya taarifa za virusi vya corona duniani kimeripoti kuwa zaidi ya watu 102,000 wamefariki duniani kutokana na virusi hivyo, lakini wataalam wengi wa afya ya umma ulimwenguni wanaamini idadi ya vifo iko juu zaidi kutokana na uhaba wa uchunguzi, vifo vinavyotokana na COVID-19 ambavyo havikuhusishwa na ugonjwa huo na vifo ambavyo haviripotiwi kutokana na watu wasiokuwa na makazi na sababu nyingine.

Marekani ni yenye maambukizi zaidi ya virusi vya corona duniani ambapo kuna zaidi ya maambukizi nusu milioni ya maambukizi milioni 1.7.Inafuatiwa na Uhispania yenye maambukizi 158,000 na Itali ambayo inamaambukizi 147,000.

Ijumaa kulikuwa na janga la vifo Marekani kutokana na virusi, ikirikodi vifo.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi cha Marekani, CDC, kimesema idadi ya vifo ni makadirio pungufu,” idadi iliyofuatilia vifo tu vilivyothibitishwa baada ya sampuli zao kupimwa.

Nchini Brazil, idadi ya vifo ilivuka 1,000 Ijumaa, na kuifanya nchi hiyo nchi ya kwanza katika eneo la Ulaya kufikia idadi hiyo.

China imeendelea kuripoti idadi ya chini ya maambukizi mapya ya virusi hivyo Ijumaa, ikisema jimbo la Hubei, ambapo virusi hivyo vilianza, ilirikodi maambukizi maambukizi,sifuri wakati maeneo mengine ya China yalikuwa na idadi ya maambukizi ya watu 46.

XS
SM
MD
LG