Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:14

Madaktari Kenya wakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi katika vyumba vya ICU


Afisa mkaguzi wa Afya akiwaonyesha madaktari namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kabla ya madaktari hao wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta ya Nairobi kuelekea katika wadi iliyowekewa karantini ya Hospitali ya Mbagathi, Alhamisi, April2, 2020.AP Photo/Brian).
Afisa mkaguzi wa Afya akiwaonyesha madaktari namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na virusi vya corona kabla ya madaktari hao wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta ya Nairobi kuelekea katika wadi iliyowekewa karantini ya Hospitali ya Mbagathi, Alhamisi, April2, 2020.AP Photo/Brian).

Madaktari nchini Kenya wanakabiliana na uhaba mkubwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona. 

Nchi inajitahidi kudhibiti janga la Covid 19 kwa kununua vifaa kwa ajili ya ICU, hasa mashine za kusaidia kupumua ambazo zinahitajika sana katika kesi nyingi za wagonjwa wenye matatizo ya kiafya.

Madaktari nchini Kenya hivi wanaangalia ujuzi wa wenzao walioko nje ya nchi ili kujitayarisha vyema na janga hili.

kabla ya virusi vya corona kuingia nchini ambavyo vinasababisha Covid 19, Dr. Wangari Waweru-Siika kwa miaka kadhaa amekuwa akifanya kazi kujibu maswali magumu kuhusu maisha na vifo ambavyo hivi sasa dunia inaulizia katika ya janga hili: ambapo mgonjwa gani sasa anapewa kitanda ICU na mashine ya kumsaidia kupumua na vifaa vingine vya kuokoa maisha nayupi asipatiwe vifaa hivyo.

Waweru-siika ni daktari bingwa na profes katika Hospitali ya Chuoo Kikuu cha Aga Khan mjini Nairobi, amekuwa mstari wa mbele kuweka miundo ya kimaadili kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa mahututi nchini Kenya.

"Unahitaji kuwa na mfumno wa wazi ambao ni tofauti na ule wa kawaida linapokuja suala na Covid. Kuna baadhi ya wagonjwa ambao katika baadhi ya taasisi kote duniani, kama wakipata Covid, hawalazwi ICU kwasababu nafasi yao ya kunusurika ni ndogo," anasema Dr. Waweru-siika.

Kenya ina kesi takriban 180 zilizothibitishwa za virusi vya corona. Watu sita wamefariki, kwa mujibu wa takwimu za karibuni kutoka chuo kikuu cha Johns Hopkins, ambacho kinafuatilia janga hili kote duniani.

Miongoni kwa kesi zote za Covid-19, asilimia 14 zitahitaji mgonjwa kulazwa hospitali na kupewa msaada wa kupumua, kwa mujibu wa muongozo wa Shirika la Afya Duniani (WHO). ingawaje asilimia 5 watahitaji kulazwa kwenye kitengo cha ICU, nchi nyingi za Afrika ICU tayari hazitoshi.

Kenya ina vitanda 158 ICU, kwa mujibu wa Kenya Healthcare Federation and Critical Care Society, ingawaje sizo ambazo zinafanya kazi. Mwezi Februari, utafiti wa chuo kikuu cha Makerere uliripoti kwamba Ugandaina vitanda 55 vya ICU. Sudan Kusini ina vitanda 24 vya ICU na mashine nne za kusaidia kupumua.

Na si ICU zote zinatumika kikamilifu nchini Kenya. Thoms Chokwe wa chuo kikuu cha Nairobi na hospitali ya taifa ya Kenyatta anasema kwamba hata katika mahospitali makubwa ya rufaa ambayo hivi karibuni yamepanua huduma za ICU, ni sehemu ndogo tu vitanda vinaweza kkutumika kwa usalama kwasababu ya uhaba wa wafanyakazi.

"Wakati wa janga kama hili hivi sasa, ndipo unabaini kuwa unahtiaji kwatalaamu wa ICU. Huwezi kuwapatia mafunzo ya haraka. Lazima uwaptie mafunzo kwa kipindi kirefu kijacho, na lazima wawepo kama rasilimali ili waweze kutumika inapohitajika," Chokwe anasema.

Kwa Waweru-siika anasema ana matumaini kuwa janga la Covid 19 linatabainisha umuhimu wa kuwa na watalaamu wa kutosha katika kitengo cha ICU nchini Kenya.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG