Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:58

COVID-19 : Boris Johnson aendelea kulazwa chumba cha mahtuti siku ya pili


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Afisa mmoja wa Uingereza amesema Jumatano Waziri Mkuu Boris Johnson anaendelea vizuri baada ya kulazwa kwa siku ya pili katika chumba cha mahtuti kwenye hospitali mmoja nchini Uingereza akitibiwa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Naibu Waziri wa Afya Edward Argar amesema Johnson yuko katika “hali nzuri na yenye matumaini.”

Waziri Mkuu amelazwa hospitali tangu Jumapili baada ya dalili zake za virusi hivyo kuendelea katika kipindi chote cha kujitenga baada ya kupimwa na kukutikana na virusi.

Uingereza, ambayo imetangaza amri ya kutotoka majumbani kwa takriban wiki mbili sasa, ina watu wenye maambukizi ya virusi vya corona waliopimwa 56,000 na vifo 6,100.

Hadi Jumatano idadi ya maambukizi duniani imefikia zaidi ya milioni 1.4, vifo ni 83,109 na watu waliopona ni 309,113.

Korea Kusini haijafuata hatua Madhubuti zilizochukuliwa na nchi nyingine za amri ya kutotoka majumbani, lakini imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza maambukizi mapya ya virusi ikiwataka watu kutokaribiana na kuamuru shule zote zifungwe.

Serikali ya nchi hiyo imetangaza maambukizi mapya 53 Jumatano, na kuendelea na kiwango kile kile cha maambukizi katika wiki hii.

Kulikuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kuwepo maambukizi Zaidi katika mji mkuu wa Seoul, na Jumatano meya wa jiji hilo alitangaza kufunga mabaa na maeneo ya starehe yanayofunguliwa usiku.

Waziri Mkuu wa Korea Kusini Chung Sye-kyun pia ametangaza kusitisha ruhusa ya visa kwa watu ambao wanatoka nchi ambazo hivi sasa zimewazuia wananchi wa Korea Kusini kuingia katika nchi zao, pia kutoa amri zinazo wakataza raia wa kigeni wanaosafari bila sababu za dharura.

Wakati huohuo Norway inaungana na Austria na Denmark na mpango wa kuanza kulegeza masharti ya kutotoka nje.

Serikali inapanga kufungua shule za chekechea Aprili 20, wakati Watoto wengine muda wao wa kurejea shuleni ni kuanzia wiki ijayo.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) bara la Ulaya ametahadharisha Jumatano dhidi ya watu kuharakisha kulegeza amri ya kutotoka majumbani iliyo kusudiwa kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

“Ni wakati muwafaka kupitia tena mara mbili au tatu juhudi zetu za pamoja katika kudhibiti maradhi haya tukiungwa mkono kikamilifu na jamii,” Hans Kluge amewaambia waandishi.

Mjini Vatican, Papa Francis amekemea wale wanaotaka kutumia janga hili kutengeneza faida ya kibiashara, akiwaombea “mioyo yao ibadilike.”

XS
SM
MD
LG