Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:06

New York yajiandaa kukabiliana na vifo zaidi, wakati maambukizi duniani yafikia milioni 1.2, vifo zaidi ya laki 2


Watu waendelea kuvaa maski katika mitaa ya New York kujilinda na kusambaza virusi vya corona pamoja na kuambukizwa. Picha hii ilichukuliwa Aprili 03, 2020.
Watu waendelea kuvaa maski katika mitaa ya New York kujilinda na kusambaza virusi vya corona pamoja na kuambukizwa. Picha hii ilichukuliwa Aprili 03, 2020.

Wakati miji mingi duniani ikiwa imebakia mitupu kutokana na amri ya kutotoka majumbani, maambukizi siku ya Jumapili yamefikia zaidi ya milioni 1.2, vifo 65,666 na watt 253,694 wamepona baada ya kuugua maradhi yanayotokana na virusi vya corona.

Marekani

Kwa upande wa Marekani ni siku 30 tu tangu mgonjwa wa kwanza kuugua kutokana na virusi vya corona,” Gavana wa New York Andrew Cuomo anayeedelea kupambana na hali ngumu ambayo imeilikumba jimbo lake. “Ni kama litaendelea katika uhai wote.

New York ni jimbo la Marekani lililoathiriwa vibaya sana na virusi vya corona, ambako imesababisha vifo zaidi ya 3,500. Wataalam wa afya ya umma wanasema muda siyo mrefu hali itakuwa mbaya zaidi, siyo tu kwa New York lakini Marekani yote pia.

Wakati Cuomo anasema kuwa jimbo hilo karibuni litafikia kilele cha janga hilo la afya, Rais wa Marekani Donald Trump ameonya Jumamosi kuwa Marekani itakabiliwa muda siyo mrefu na wiki mbili za hali ngumu ya maambukizi ya virusi.

“Kutakuwa na vifo vingi,” Trump amesema.

Hospitali za Marekani zimekuwa zikipambana na virusi vya corona katika hali ya kutokuwa na vifaa vya kutosha.

Mahospitali yamekuwa yakiomba vifaa vya kupumulia kwa ajili ya wagonjwa na vifaa vya kujilinda ambavyo madaktari na wafanyakazi wa afya wanavaa ili kuepusha kusambaza maradhi kati yao na wagonjwa.

New York imepokea meli yenye vifaa 1,000 vya kusaidia kupumua Jumamosi kutoka China.

“Huu ni msaada mkubwa na utaleta mabadiliko makubwa kwetu,” Cuomo amesema.

Cuomo amesema pia watu 85,000 wamejitolea kusaidia mji wa New York kukabiliana na virusi na atasaini amri ya kiutendaji kuruhusu madaktari wanafunzi ambao wanatarajiwa kumaliza masomo yao kipindi cha karibuni wapewe shahada zao mapema ili waanze kutoa matibabu.

Mvutano kati ya Trump and Majimbo

Baadhi ya majimbo yamekuwa na mvutano na White House kwa sababu uongozi wa Trump haujaanzisha muelekeo wa pamoja kama taifa kukabiliana na virusi hivyo, na kutaka kila jimbo la Marekani kutengeneza mkakati wake kutafuta vifaa vya tiba na madawa kupambana na janga la virusi.

Gazeti la Washington Post limeripoti White House ilifahamishwa rasmi juu ya mlipuko huo uliotokea China Januari 3, lakini uongozi wa Trump ulichukuwa siku 70 kutambua kuwa mlipuko huo ni janga hatarishi hali ilioko hivi sasa.

DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumapili kumekuwa na vifo vitiate vipya na maambukizi zaidi ya 23.

Spain

Uhispania, ambayo ina maambukizi zaidi ya 126,000 na vifo takriban 12,000, inapanga siku 15 zaidi za kutotoka nje, hadi Aprili 26.

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema Jumamosi atalitaka bunge kuongeza amri ya kutotoka majumbani kwa mara ya pili baada ya kuongeza muda hadi Aprili 11.

Itali

Itali, ni ya pili kuathirika zaidi na virusi vya corona Ulaya baada ya Uhispania, ilikuwa na zaidi ya maambukizi 11,000 ya wafanyakazi wa afya walioambukizwa COVID-19, kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Taifa na jumuiya ya madaktari.

Vikundi hivyo vimesema kuwa madaktari 73 wamefariki kutokana na virusi hivyo. Maambukizi kati ya wafanyakazi wa afya ni takriban asilimia 10 ya maambukizi yote Itali.

Uingereza

Waziri wa Sheria ya Uingereza amesema Jumamosi kuwa maelfu ya wafungwa wataachiwa huru katika wiki mbili ikiwa ni sehemu kubwa ya kampeni ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Uingereza imeripoti vifo 708 kwa usiku mmoja, ikiongeza idadi ya vifo katika nchi hiyo kufikia zaidi ya watu 4,300.

Wizara imesema kuwa wafungwa watakuwa wakifuatiliwa kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki kuhakikisha wanakaa majumbani na wanaweza kurudishwa jela “ endapo watakiuka amri hiyo.”

Ufaransa

Jeshi la Ufaransa limeanza kuwahamisha wagonjwa katika hospitali mbalimbali nchini katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi ndani na maeneo yanayo izunguka Paris. Ndege za kujeshi, helikopta na treni zinawasafirisha wagonjwa katika maeneo yaliyo kuwa na maambukizi machache magharibi ya Ufaransa.

Zaidi ya vifo 7,500 na maambukizi 90,000 yameripotiwa Ufaransa.

China

China imetekeleza maombolezo ya kitaifa kwa dakika tatu Jumamosi, wakati bendera zikipeperushwa nusu mlingoti, na ving’ora vikilia kuwakumbuka wahanga wa COVID-19 na wafanyakazi wa afya waliokufa wakiwa mstari wa mbele katika taifa hilo la Asia kupambana katika kuokoa Maisha ya wagonjwa.

Virusi vya corona viliibuka mwisho wa mwaka 2019 huko China katika jimbo la Hubei, na kuua zaidi ya watu 3,300.

XS
SM
MD
LG